25 Agosti 2017
Ni msimu mwingine wa Soko la Wazi la Mkulima
Market maarufu kama Mkulima Soko. Tunakukaribisha kuungana na wazalishaji na
wachakataji bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji kuona wazalishaji
kutoka kila pembe ya Tanzania. Katika Mkulima Soko utapata fursa ya kuona,
kupata elimu na kununua bidhaa bora zinazozalishwa Tanzania.
Soko hili la Wazi litafanyika kuanzia tarehe
30 Agosti hadi 2 Septemba 2017 (Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi). Karibu
ujifunze ufugaji wa sungura, samaki na nyuki. Kama kawaida soko litafanyika
kwenye Maegesho ya Magari ya Research Flats, mbele ya Jengo la Ndaki ya Kilimo
na Teknolojia za Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Msimu huu kutakuwa na
wazalishaji wapatao 60 watakaoleta bidhaa mbalimbali fresh na zilizochalatwa.
Katika soko hili kutakuwa na mambo makubwa
manne:
1. Mkulima
Market itazindua rasmi kidokozi (app) pamoja tovuti yake ya mkulimamarket.com
ili kuwezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa zilizopo katika sekta
ya Kilimo, Uvuvi, Ufuaji na Uwindaji.
2. Uzinduzi
wa masoko ya wazi ya kila mwisho wa wiki yatakayofanyika kwenye eneo la Organic
Farmer Supermarket iliyopo eneo la Kijitonyama mita 300 toka kwenye taa za
Sayansi, mkabala na Hoteli ya Colubus. Hivyo basi wakati wa soko la wazi,
wazalishaji watapata fursa ya kujiunga na mtandao huu mkubwa wa wazalishaji wa
bidhaa zenye ubora kutoka shambani hususani nyanya, vitunguu, pilipili hoho,
karoti, viazi, mchele, unga wa mahindi, kuku samaki na asali.
3. Uhabarishaji
kuhusu huduma mpya ya kupata bidhaa mlangoni kwako iitwayo Mkulima Basket kwa
kushirikiana na Organic Farmer Supermarket.
4. Pia
tutakuwa elimu kuhusu ufugaji sungura itakayotolewa Uhuru Rabbits. Pamoja na kutoa elimu kuhusu ufugaji wa
sungura wataendesha onesho la kuonja nyama choma ya sungura.
Tunamkaribisha kila mwana Dar es Salaam kuja
kuona ubunifu na maendeleo yanayotokana na biashara katika sekta kilimo nchini
Tanzania. Kama kawaida kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na michezo ya watoto.
Hakuna kiingilio
Unaweza
kuwasiliana na Mratibu kupitia namba 0767 254 887 au 0629 042 678 au kwa
kuandika barua pepe kupitia mkulimamarket@gmail.com au kwenye mitandao ya
kijamii ya twitter, facebook, instagram na youtube.
Shukrani za kipekee kabisa ziende kwa
Kilimanjaro Audiovisual Services (KAVS), Michuzi Blog, Baraza la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na TanTrade kwa kuendelea kuuunga mkono kazi za
Mkulima Market.
Eid Mubarak
1 comment:
Ever wanted to get free Facebook Followers?
Did you know that you can get them ON AUTO-PILOT AND ABSOLUTELY FOR FREE by getting an account on Like 4 Like?
Post a Comment