Watemi
wa Kisukuma Kanda ya Ziwa Victoria na viongozi wa Chama Cha Watu Wenye
Ualbino nchini Tanzania( Tanzania Albinism Society -TAS) wamefanya usafi
wa mazingira kisha kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Watemi
hao wakiongozwa na Katibu Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi
Charles Balele Itale wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza
walitembelea kituo hicho leo Jumamosi Julai 8,2017.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba
alisema chama hicho kimekuwa na ushirikiano mkubwa na machifu wa kanda
ya ziwa hicho kuamua kushiriki nao katika kufanya usafi wa mazingira
katika kituo cha Buhangija.
“Malengo
ya kuja hapa kwanza ni kuunga mkono serikali ya awamu ya tano kuhusu
masuala ya usafi,pili ni kuwapa ujumbe watoto hawa kuwa wawe na
utamaduni wa kufanya usafi hata wanaporudi kwenye familia zao,tatu
tumekuja kula chakula cha pamoja na watoto hawa ili kuonesha kuwa tuko
pamoja nao”,alieleza Temba.
Temba
alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuchunguza utitiri wa mashirika
yaliyoanzishwa nchini ambapo sasa yapo zaidi ya 10 na kufuatilia vituo
mbalimbali vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwahudumia watu wenye ualbino
hususani watoto kwani sasa vipo takribani 20 lakini wahusika wa vituo
hivyo hawasaidii walengwa.
Temba
alisema mashirika mengi yamekuwa yakijikita katika kupiga vita mauaji
ya watu wenye ualbino huku yakisahau kuwa watu wenye ualbino
wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa elimu na saratani
ya ngozi ambayo imekuwa ikiua watu wengi wenye ualbino.
Katibu
Watemi wa Kisukuma Kanda ya Ziwa, Mtemi Charles Balele Itale wa Bujashi
wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza alimpongeza mwenyekiti wa Chama cha Watu
wenye Ualbino kuwakutanisha pamoja katika kituo hicho. “Juhudi hizi
zinaonesha jinsi tunavyowatambua,tunavyowapenda na tunavyowajali watu
wenye ualbino,kwa hiyo katika nafasi zetu za nyadhifa mbalimbali
tunajitahidi kuelimisha na kuwezesha jamii iwatambue,iwajali,iwapende na
kuwapokea katika jamii na watoto warudi kwenye familia zao na kuishi
kama watoto wengine”,alieleza Mtemi Balele.
“Nimefurahishwa
na taarifa ya uongozi wa kituo hiki kuwa sasa watoto wameanza kwenda
likizo kuwaona wazazi wao,hili ni jambo jema sana,Sisi machifu tuna
jukumu letu ni kuielimisha jamii
iwapokee,iwakubali,isiwanyanyase,isiwanyanyapae hivyo sisi kwa
kushirikiana na TAS tutashirikiana katika kutafikia hayo
malengo”,aliongeza Mtemi Balele.
Awali
akizungumza katika kituo hicho,Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi
Buhangija, Frola Kakutebe alisema kati ya watoto wenye ualbino
140,waliopo katika kituo hicho,72 wameenda likizo na 68 wamebakia
kituoni baada ya shule kufungwa kinyume na miaka ya nyuma ambapo watoto
hao walikuwa hawaendi likizo kuonana na ndugu zao.
Mwalimu
Mkuu wa Shule hiyo,Selemani Kipanya aliiambia Malunde1 blog kuwa,sasa
Kituo hicho kimepoteza sifa ya kuitwa kituo bali ni shule kwani tofauti
na siku za nyuma hivi sasa watoto wanaoishi hapo wote wanasoma shule na
wanaishi katika mabweni yaliyopo katika shule hiyo.
Katibu
Mtendaji wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS
taifa,Mussa Mussa akizungumza katika kituo/Shule ya Msingi Buhangija
katika manispaa ya Shinyanga.Kulia ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa
Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu
mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele.Kushoto ni Mwalimu Mlezi wa Shule ya
Msingi Buhangija, Frola Kakutebe-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1
blog
Katibu
wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa
Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale
akizungumza katika kituo cha Buhangija.Kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba
Mtemi Balele akizungumza katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija.
Kushono
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa,
Nemes Temba akifuatiwa na Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza
‘Ng’wanza (katikati),kulia ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani
Simiyu wakiwa eneo la tukio.
Kushoto
ni Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu,akifuatiwa na Mtemi
Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga,kulia ni
Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba
akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliiomba serikali kuona
umuhimu wa kuwapa nguvu viongozi wa kimila kama zamani kwani
wanazungukwa na watu wengi hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kuleta
mabadiliko katika jamii.
Watoto,walimu na maafisa kutoka TAS wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza katika kituo cha Buhangija.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes Temba akisisitiza jambo.
Watoto na maafisa kutoka TAS wakiwa eneo la tukio
Katibu
wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa, ambaye ni chifu/mtemi wa
Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza Charles Dotto Balele Itale akila
chakula na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija katika manispaa
ya Shinyanga.
Mtemi
Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akila chakula na watoto wa
wanaolelewa katika kituo cha Buhangija,ambapo wapo wenye
ualbino,wasiosikia na wasioona.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS taifa, Nemes
Temba,Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu na Mtemi Charles
Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga wakila chakula na
watoto kituo cha Buhangija.
Mtemi Charles Gagambaseni Dogani wa Seke – Kishapu mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
Watemi
na Viongozi wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania -TAS
wakiendelea kula chakula na watoto katika kituo cha Buhangija.
Mtemi Charles Lubasha Kimwaga Kaswende wa Luhumbo mkoani Shinyanga akila chakula na watoto.
Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza ‘Ng’wanza akila chakula na watoto.
Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner akila chakula na watoto.
Kushoto
ni Katibu wa Umoja wa Watemi wa Kisukuma kanda ya Ziwa,Charles Dotto
Balele Itale ambaye ni Mtemi wa Bujashi wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza
akifuatiwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka chama cha watu wenye
ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torne (katikati) na Afisa Programu
kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward wakifanya
usafi katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Buhangija
manispaa ya Shinyanga.
Mtemi Wenceslaus Seni wa Kanadi mkoani Simiyu akifanya usafi karibu na choo wa watoto katika kituo cha Buhangija.
Mtemi Nyamilonda III Mikomangwa Aron wa Mwanza ‘Ng’wanza akiweka uchafu kwenye ndoo.
Kulia
ni Afisa Programu kutoka Chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin
Edward na Mwalimu Mlezi wa Shule ya Msingi Buhangija, Frola Kakutebe
wakifanya usafi katika kituo cha Buhangija.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment