Sunday, July 9, 2017

RAIS MSTAAFU BENJAMINI WILLIAM MKAPA AFUNGUA JENGO LA UPASUAJI KWENYE KITUO CHA AFYA CHA NKOMO WILAYANI ITILIMA

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo kilichopo kijiji cha Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu,kulia ni Balaozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo hilo limejengwa na Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 270.
Rais Mstaafu akiangalia moja ya vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi wa jengo hilo kwa asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali wananchi wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata huduma za namna hiyo.
Jengo hilo la upasuaji linavyoonekana
Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey Nyaluke (mwenye fulana ya jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika kushuhudia ufunguzi wa jengo hilo
Rais Mstaafu akicheza mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka na kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Daudi Njalu



Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi(hawapo pichani)ambapo alisema katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Wilaya ya Itilima ametengewa kiasi cha shilingi milioni 584 kwa ajili ya ununuzi wa dawa ukilinganisha na bajeti iliyopita ya mwaka 2016/2017 ambapo shilingi milioni 315 zilitengwa.
Wananchi wa kijiji cha Mwalushu wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Nkomo.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ufunguzi huo akiwepo mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa

No comments: