Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) akikata
utepe kama ishara ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme
Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa Mwanza.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akielezea mikakati ya
serikali ya kupeleka umeme katika vijiji na vitongoji vyote mkoani
Mwanza kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu
kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akielezea hali ya umeme katika mkoa huo kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga
(kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini Dkt. Gideon Kaunda
(kulia) wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) kwenye uzinduzi
wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa
Mwanza uliofanyika katika kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani
humo tarehe 13 Julai, 2017.
Sehemu
ya wananchi wa kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani Mwanza
wakifuatilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa inatolewa na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ( hayupo pichani) kwenye uzinduzi
wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwa mkoa wa
Mwanza uliofanyika katika kijiji cha Nyamatala wilayani Kwimba mkoani
humo tarehe 13 Julai, 2017.
Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa akieleza jambo kwenye uzinduzi huo.
Sehemu
ya wataalam kutoka mkandarasi atakayejenga miundombinu ya umeme katika
mkoa wa Mwanza kupitia Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu
ya Tatu wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kwenye uzinduzi huo.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (wa tano kulia) na
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa sita kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na wabunge, watendaji kutoka Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na viongozi wengine wa
kitaifa mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment