Tuesday, July 4, 2017

TIMU YA TAIFA YA CRICKET YARUDI NCHINI NA VIKOMBE VIWILI NA MEDALI KUTOKEA DUBAI KWENYE MASHINDANO YA DUNIA


Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cricket waliotoka katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Dubai ambapo walishiriki mashindano ya Dunia yajulikanayo kama Memon World Cup na kufanikiwa kuchukua nafasi ya tano.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket wakiwasili nchini kutoka Dubai walikokwenda kushiriki mashindano ya Dunia ya Memon World Cup na kufanikiwa kushika nafasi ya tano na kurudi na Vikombe Viwili na Medali ,ambapo mashindano hayo yalijumuisha timu 12 kutoka nchi mbalimbali zilizofuzu
 Sehemu ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket  wakiwa na mizigo yao ndani ya uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam
 Wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket wakionyesha vikombe walivyopata na Medali katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo
 Viongozi na Wachezaji wa mchezo huo wakiwa wanatoka na mizigo ndani ya uwanja wa  Kimataifa wa Ndege wa JK Nyerere wakitokea nchini Dubai kwenye mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Cricket ambapo Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tano

No comments: