Monday, July 31, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TLEVISHENI

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameonya kuwa Tanzania sio lango la kupitisha dawa za kulevya na kutaka ulinzi kuimarishwa maeneo ya mipaka ya nchi. https://youtu.be/wSFAF3ciXWE

SIMU.TV: Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Nemeles Mbatia ameuawa kwa mlipuko wa  bomu na askari wawili kujeruhiwa kutokana na mgogoro wa kugombania eneo la kuchimba madini ya Tanzanite huko Mererani mkoani Manyara. https://youtu.be/StWgN-Sexck

SIMU.TV: Serikali mkoani Mwanza imewaadhibu vigogo saba ambao wanasadikiwa kusababisha ubadhirifu wa fedha za maendeleo. https://youtu.be/ScIqR1nd0KE

SIMU.TV: Wakandarasi wanaojenga majengo ya chuo cha ualimu Kitangiri kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara wamejikuta wakijenga majengo hayo chini ya usimamizi mkali baada ya kulalamikiwa kuwadharau viongozi wa wilaya hiyo. https://youtu.be/F76JcllS2qA

SIMU.TV: Halmashauri na wakala wa barabara hapa nchini wameagizwa kutekeleza agizo la serikali la kusaidia vikundi mbalimbali vya kijamii kwa kuvipa ajira. https://youtu.be/u7kB-zhpOmw

SIMU.TV: Taasisi ya utafiti na kilimo ya Naliendele mkoani Mtwara imetoa mafunzo ya kilimo cha kisasa cha zao la korosho kwa jeshi la magereza ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo hapa nchini. https://youtu.be/4_l-VFITn7k

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezindua meli  mbili za mizigo katika bandari ya Kiwira ziwa Nyasa wilayani Kyela  na kutahadharisha meli hizo kutumika vyema. https://youtu.be/9BwgNuS4y6A

SIMU.TV: Wananchama wa klabu ya soka ya Simba wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la wadhamini Hamis Kilomoni wamegoma kutohudhuri mkutano mkuu ulioitishwa na viongozi wanaokaimu nafasi za viongozi wa juu kwa kuwa mkutano huo ni batili. https://youtu.be/FAoI5Y1u0IE

SIMU.TV: Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mbio za baiskeli na ngoma za asili mkoani Simiyu august sita. https://youtu.be/ywffnrNWE7U

SIMU.TV: Viane Kundi mkazi wa mjini Iringa amejinyakulia milioni 20 kwenye droo ya bahati na sibu ya BIKO iliyo chezeshwa leo jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/Ic4rQJfXE_c

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania imetenga fedha zaidi ya shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya kumaliza kero ya maji katika  wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya; https://youtu.be/BVFZW3nMAps

SIMU.TV: Magunia 560 ya mkaa na mbao 1600 zilizokuwa zimevunwa na kusafirishwa bila kibali zimekamatwa huko wilayani Songea mkoani Ruvuma; https://youtu.be/MFEwvcqlURw

SIMU.TV: Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Amour Amour amewaagiza wakuu wilaya, viongozi wa kata na vijiji kuwafichua wote wanaoharibu misitu; https://youtu.be/fX8NnK0DWtY

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Steven amepiga marufuku biashara ya usafirishaji wa magunia ya vyakula usiku wa manane kwa lengo ya kukwepa kodi; https://youtu.be/SSQLfNgvGrQ

SIMU.TV: Meneja wa mamlaka ya usimamizi wa bima kanda ya kati Stella Rutaguza amesema sheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wanaotoa bima feki; https://youtu.be/_oa-1NI_PfY

SIMU.TV: Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya Takwimu Dr Albina Chuwa amewatahadharisha wadadisi wa kutathamini mpango wa TASAF kuwa makini na taarifa zao; https://youtu.be/o6UJomBM4DA

SIMU.TV: Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Tanapa Jenerali George Waitara amesema suala la kudhibiti ujangili nchini Tanzania ni la kila mmoja wetu; https://youtu.be/prJ3NDqOIBE

SIMU.TV: Baadhi ya wakulima katika tarafa ya Nshamba wilayani Muleba mkoani Kagera wamesema utaalamu wa kutumia mbolea asilia umewasaidia kuboresha mazao yao; https://youtu.be/P7lbU_zWW54  

SIMU.TV: Timu ya jeshi la Lugalo imeibuka mabingwa katika mashindano ya taifa ya mchezo wa Vishale kwa wanaume katika mashindano yaliyofanyika huko Mbeya; https://youtu.be/IhRoD8XLyng

SIMU.TV: Chama cha mchezo wa riadha Tanzania RT kimetolea ufafanuzi kitendo cha kumuacha mchezaji Said Makula na kumchukua Stephano Uche; https://youtu.be/VBceFjKA0Os

SIMU.TV: Baraza la wazee wa Klabu ya Simba limesema kuwa suala la kutaka kuimilikisha klabu ya Simba kwa mtu mmoja kamwe haliwezekani; https://youtu.be/6nheLJFxd44

SIMU.TV: Naibu spika wa bunge la Tanzania Dr Tulia Ackson anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Utamaduni la mkoa wa Simiyu; https://youtu.be/2-XifHd9-1U

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa klabu ya Real Madrdi na kunyakua kombe la ICC; https://youtu.be/YpafzjYJ5Yw

No comments: