Jumuiya ya Watanzania wa Reading {Tanzania Reading - Berkshire Association- } imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia Kwa mujibu wa Katiba yake halali siku ya Jumamosi ya tarehe 29 July 2017 katika jiji la Reading.
Zoezi la Uchaguzi lilisimamiwa kikamilifu Kwa mujibu wa Katiba halali ya Jumuiya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi 2017 Ndugu Bernard Chisumo pamoja na timu yake chini ya Makamu Mwenyekiti na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Hussein Chang'a.
Katika hotuba yake fupi Ndugu Chang'a alisisitiza umuhimu wa wajumbe kuheshimu muongozo wa Jumuiya na kufanya shughuli zote za kwa kufuata muongozo waliojiwekea na kutokukubali kuyumbishwa na watu wachache wenye malengo binafsi.
*Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK {Great Britain & Northern Ireland}, Ndugu Abraham Sangiwa. ambaye alisindikizwa na Makamu Mwenyekiti TZUK, Bi. Mariam Seif
Katika wosia wake kwa Watanzania wa Reading Ndugu Sangiwa alisisitiza kuwa na umoja na mshikamano kwa Watanzania wote wanaoishi Reading- Berkshire na kuelezea kwa ufasaha jinsi TZUK inavyofanya shughuli zake kwa kushirikiana na jumuiya zote za mikoa hapa UK.
Ndugu Sangiwa alielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kwa kushirikiana na Jumuiya mbalimbali za Watanzania wanaoishi nje katika nchi mbalimbali duniani kupendekeza sera ya Diaspora kwa pamoja itakayotoa majibu katika masuala mbalimbali yanayowagusa Watanzania Ughaibuni na mchango wao mkubwa kwa nchi yao mama "TANZANIA", unavoweza kuwa katika mfumo utakaoleta manufaa makubwa kwa nchi katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo na huduma kwa jamii.
"Tunahitaji kulinda na kutangaza utamaduni wetu na vivutio vya utalii kwa kuhakikisha vizazi vyetu ughaibuni vinanapata misingi muhimu na mafunzo kuhusu Tanzania. Ni muhimu sana kujenga "Model" itakayofanya TAIFA letu kufaidika na vizazi hivi vitakavokuwa na " Exposure " ya kimataifa katika nyanja mbalimbali zenye manufaa makubwa kwa nchi yetu, alisisitiza Ndugu SANGIWA.
VIONGOZI WAPYA WALIOCHAGULIWA KUONGOZA JUMUIYA YA WATANZANIA READING - BERKSHIRE NI KAMA IFUATAVYO:
MWENYEKITI NI NDUGU JOE J.E WARIOBA, MAKAMU MWENYEKITI NI Bi. LAURA BANDUKA, KATIBU MKUU NI Bi. Raya Walker, NAIBU KATIBU {KAIMU}, Bw. Peter Owino, MTUNZA HAZINA ni Bi. FLORA DICKSON, wakati MTUNZA HAZINA MSAIDIZI ni Ndugu Elijah Mwamunyange.
WAJUMBE SITA NI Peter Owino, MOHAMMED Upete, Paul Onyango, Geofrey Mumu, Evelyne Furzei na Dorine White, wakati Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu (AUDITOR) ni Eliud Mwijarubi.
Pia kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae.
Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK
Asanteni sana
Uongozi: TA READING - BERKSHIRE*Kwa kushirikiana na
Tanzania Diaspora Community/Association - United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland
Makamu mwenyekiti mpya Bi. Laura Noe akinadi sera zake
Bi. Raya Walker akijinadi na kuomba kura kwa wanachama
Hussein Chang'a
Katibu Bi. Raya Walker na Mwenyekiti Ndugu Joe J.E Warioba wakibadilishana mawazo
Ndugu Mohamed Upete akitimiza haki yake ya kupiga kura
Makamu na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu ndg Hussein Chang'a akitimiza haki yake ya kupiga kura kama mwanachama hai
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TA READING- BERKSHIRE Ndugu Bernard Chisumo pamoja na Katibu wa TZUK Ndugu Gerald Lusingu wakifuatilia mambo kadhaa katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya.
Masanduku ya kura yakisubiri kula kura
Wajumbe na Wanachama wakiwa makini
Meza kuu na Wajumbe na Wanachama
Makamu na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Hussein Chang'a akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa TA Reading- Berkshire aliyechaguliwa Ndugu Joe J.E Warioba. Kushoto ni Katibu mpya Bi Raya Walker na kulia ni Makamu mwenyekiti mpya Bi. Laura Noel
Ndugu Hussein Chang'a Makamu na Kaimu Mwenyekiti Mstaafu akikabidhi Uongozi Mpya taarifa zote muhimu za Jumuiya kwa Katibu Mpya Bi. Raya Walker
Mtunza Hazina Bi. Flora Dickson akimkabidhi ripoti ya Fedha na Akaunti ya Jumuiya Mwenyekiti Mpya wa TA READING BERKSHIRE Ndugu Joe J.E Warioba |
Viongozi wa TZUK na TA READING BERKSHIRE
Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Uchaguzi TA READING- BERKSHIRE na Uongozi wa TZUK
No comments:
Post a Comment