Sunday, July 16, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia viongozi sita wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa kosa la kufanya maandamano na kuzua vurugu. https://youtu.be/WhH8AWpLQBA

Mamlaka ya mapato TRA wilayani Njombe imevifungia vituo sita vya mafuta kati ya saba vilivyopo wilayani humo kwa kosa la kutofunga mashine za kieletroniki za kukusanyia mapato. https://youtu.be/rjuA5hwrRAA

Naibu waziri wa nishati na madini Dr Medadi Kalemani ameagiza mradi wa usambazi umeme vijijini REA kukamilika ndani ya miaka miwili kwa mkoa wa Mwanza. https://youtu.be/UYr9_djY73Y

Bwawa la Nyumba ya Mungu linalounganisha mikoa ya Kilimanjaro na Manyara lipo hatarini kukauka na kuathiri uzalishaji umeme pamoja na shughuli nyingine za kibinadamu. https://youtu.be/3DiuOzPcxvI

Uongozi wa chuo cha kiteknolojia cha reli cha Tabora umeombwa kukisajili chuo hicho na kuwajengea uwezo wanafunzi ili waweze kusimamia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa. https://youtu.be/fMqFange57A

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars imelazimishwa sare ya goli moja kwa moja dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda Amavubi kwenye mchezo uliopigwa jana katika uwanja CCM Kirumba Mwanza. https://youtu.be/YU2FraHNrO4

Wazee wa klabu ya Simba wameilamu kamati ya utendaji na usaji ya klabu hiyo kwa kile walichosema ni kusajili kinyemela katiba ya simba kinyume na utaratibu. https://youtu.be/y6fkyaYn-aY

Katibu mkuu wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo Pofesa Elisante Ole Gabriel amewataka waandaji wa tamaza la muziki la Jahazi maarufku kama ZIFF kuwajengea washiriki uwezo wa kuandaa filamu zenye ubora ili kulitangaza soko la filamu kimataifa. https://youtu.be/HnSqyx2q-38

Kampuni ya Msama Auction Mat imetoa muda wa wiki moja kwa wote wanaodurufu kazi za wasanii kuacha mara moja. https://youtu.be/tk3kJ__vDU4

Mashindano ya wazi ya gofu ya Moshi Open yameanza kutimua vunbi katika viwanja vya Moshi Club ambapo wachezaji wengi wamejitokeza kushiriki. https://youtu.be/gyp-LcnLeS0    

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia katibu mkuu wa CHADEMA Dr Vicent Mashinji na viongozi wengine sita kwa kosa la kufanya maandamano bila kibali. https://youtu.be/pCFndOy07nY

Vikundi 106 vya wanawake wanaounda VICOBA mkoani Lindi na  Mtwara vimewezeshwa na mikopo yenye zaidi ya shilingi Bilioni moja. https://youtu.be/b5rdrodii-E

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametembelea na kukagua ujenzi wa Gati mkoani Lindi na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo. https://youtu.be/08oZA6H0kfM

Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania TAA kuhakikisha viwanja vya ndege vilivyo boreshwa vinajitegemea na kujiendesha vyenyewe. https://youtu.be/0VYYbaqwXUE

Wizara ya nishati na madini imemuagiza mkandarasi anaetekeleza mradi wa REA awamu ya tatu mkoani Mwanza kukamilisha mradi huo ndani ya miezi 16. https://youtu.be/91rpClbJ_CQ

Watanzania wametakiwa kujenga uzalendo kwa kusimamia na kulinda rasilimali zinazopatikana hapa nchini kwa maendeleo ya taifa. https://youtu.be/u2B8qY18x58

Timu ya taifa Taifa stars imetoshana nguvu na timu ya taifa  ya Rwanda Amavubi baada ya kufungana bao moja kwa moja kwenye mchezo wao uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza. https://youtu.be/bd8M9KrXYdo

Mabondia watatu wa Tanzania wanatarajiwa kuwakabili mabondia kutoka DRC  Malawi na Zambia siku ya julai 22 mwaka huu katika ukumbi wa Dar Live. https://youtu.be/C6CyWGqv8Gs

No comments: