NA EVELYN MKOKOI
Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.
Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa mahakamani.
“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.
Aidha Mpina alisema ukiachilia mbali uharibifu wa Miundo Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa takribani muda wa wiki mbili.
“Mabomba haya yalikuwa chini ya mchanga lakini kwa sasa hivi yananing’inia kutokana na uchimbaji wa mchanga na mto unazidi kupanuka na maji yanakwenda kwenye makazi ya watu na kusababisha mafuriko, na madhara kwa miundombinu mingine kama vile ya umeme na barabara ambapo serikali imeijenga kwa gharama kubwa”. Alisisitiza Mpina
Alongeza kwa kusema kuwa hakuna mtu yoyote atakaye ruhusiwa kuchimba mchanga katika maeneo yasiyo ruhusiwa na wanachi wajihepushe na uharibifu wa mazingira Mpina alisisitiza kuwa serikali haizuii wananchi kuchimba mchanga bali inakataza wanachi kuchimba mchanga kiholela na kuharibu mazingira.
Naibu Waziri Mpina alisema kuwa uungwaji mkono wa sehemu nyingine ya serikali kama vile Halmashauri na vyombo vingine vya ulizi na usalama ni mkubwa na ndo maana katika opareshi hiyo hawakuweza kukuta shughuli zozote zikiendelea katika muda huo,na wahalifu wameanza kuona kuwa serikali haina mzaha na ndiyo maana team ya oparesheni hiyo imekuwepo katika eneo la tukio kwa muda huo wa usiku.
“Oparesheni hii ni agizo na zoezi hili litaenda Nchi nzima, na tumeanzia Dar es Salaam , Halmashauri zote zinatakiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kufanyika kwa shughuli hii.” Aliongeza Mpina.
Aliwaasa viongozi wasingojee Waziri NEMC au wa Viongozi wajuu kuwatembelea na kufanya zoezi hili.
Kwa upande wake Afisa kutoka DAWASA Bwana Abel Chibelene wao kama wamiliki wamiundombinu hiyo ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wamefanya jitihada za kutosha kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzai na usalama, na kufikia hatua ya kuweka walinzia katika miundombinu hiyo lakini bado wananchi wamekuwa wakiendelea na shugulizi hizo ambazo si salama kwa mazingira na miundombinu hiyo muhimu ya maji.
Opareshi hiyo ya kamata kamata ya wachimba mchanga, imeanzishwa na Naibu Waziri Mpina na kuwa ni agizo kwa Halmashauri zote na miji nchini kutekeleza zoezi hilo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi akiwasikiliza maafisa wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge akieleza kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi katika eneo la Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo Umeharibu eneo ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na kuhudunia seheu ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba ambalo lipo hatarini kuharibika.
Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenje (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto Mpigi ( haipo Pichani, iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)
No comments:
Post a Comment