Wednesday, July 12, 2017

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI SHINYANGA

Na Robert Hokororo, Kishapu

Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 umepokelewa kimkoa kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kutoka Simiyu na kuzindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 3.7.

Katika mapokezi hayo Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini alimkabidhi mwenzake wa Shinyanga, Albert Msovela ambaye alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu.
Katika mbio hizo jumla ya miradi 12 ilizinduliwa ikiwemo ya kituo cha mafuta wenye thamani ya sh. milioni 337 kutoka kwa mjasiliamali Kija Ng’wani na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na unga wa mahindi sh. 244.
Mingine ni mashine ya kukoboa mpunga na kuweka katika madaraja sh. milioni 535.8 na ufugaji ng’ombe sh. milioni 400 ya mjasiliamli Mabela Masolwa pamoja na eneo la viwanda  lenye ekari 278 ambao thamani yake ni sh. bilioni 1.1.
Mradi wa ujenzi wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria sh. milioni 755 uliofadhiliwa na shirika la Investing in Children and their Society (ICS), nyumba za walimu sh. milioni 55.8 uliofadhiliwa na mgodi wa Mwadui.
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iligharamia mradi wa pikipiki kwa vijana wajasiliamali wenye thamani y ash. Milioni 21, hudni zenye thamani y ash. Milioni 10.5 kwa wanawake wajasiliamali na utengenezaji bidhaa za ngozi wa Badimi sh. milioni 20.    
Akizungumza wakati wa mbio hizo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour aliwataka Watanzania bila kujali tofauti zao kuuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kulinda rasilimali zilizopo nchini.
Alisema taifa litaongozwa kwa kufanya kazi kwa bidii ili tufikie malengo na maendeleo huku akiongeza kuwa tumezunguzkwa na mito na ardhi yenye rutuba ya hivyo wananchi wajitume.
Alipongeza wilaya kwa kuhakikisha inakuwa na viwanda huku akiwataka wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa wilayani badala yake kuwa tegemezi kwa bidhaa za kutoka nje ya nchi ili kukuza uchumi wa taifa.
Amour aliasa miradi inayozinduliwa na Mwenge iwaguse wananchi na waisimamie ili kuleta tija na ufanisi huku akipongeza pia kwa mapambano dhidi ya Ukimwi na rushwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela kwa ajili ya kukimbizwa wilayani humo.
 Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa eneo la Maganzo wilayani Kishapu wakati ukiendelea kizindua miradi ya maendeleo. Kulia mbele ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akitoa hamasa kwa wananchi. 
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akijaza mafuta katika gari ikiwa ni katika uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta kata ya Kishapu wakati wa mbio za Mwenge wilayani.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya maji mwanachi wa kata ya Maganzo wilayani Kishapu wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita kuzindua mradi wa maji ya Ziwa Victoria.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (wa tatu kulia) akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenge kijiji cha Kinampanda kata ya Shagihilu wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kimkoa. Wengine pichani kuanzia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kiongozi wa mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (katikati) akicheza na ngoma ya wananchi wa jamii ya Kitaturu eneo la mapokezi ya Mwenge.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akiweka nafaka ya mahindi katika mashine ya kusaga unga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kiwanda kidogo cha kusindika alizeti na kusaga unga wakati wa mbio za Mwenge zilipopita kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga jana.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akikagua mojawapo ya mashine za kusaga nafaka katika eneo la mradi kwa mjasiliamali Mabela Masolwa Mhunze wilayani humo.
 Watumishi kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu kushoto mwanasheria wa wilaya, Wilson Nyamunda na Mweka Hazina wa wilaya, Deus Ngelanizya wakicheza ngoma wakati wa shamrashamra za mbio za Mwenge.
 Mwenyekiti wa halmashauari ya Kishapu, Boniphace Butondo akicheza ngoma wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kijiji cha Kinampanda.
 Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akisoma risala wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru mkoani humo. Wengine pichani kuanzia kushoto ni viongozi mbalimbali kuanzia kushoto Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhil Nkulu, 
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
 Mganga Mkuu halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joseph Shani (kulia) akitoa maelezo kuhusu Mfuko wa Afya wa CHF iliyoboreshwa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge alipotembelea banda hilo kwenye eneo la mkesha, Maganzo.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour (katikati) akizungumza katika eneo la mradi wa kusindika mafuta ya alizeti na kusaga unga wa mahindi kata ya Mwamalasa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba.
 Mkimbiza Mwenge kitaifa, Frederick Ndahani akizungumza katika eneo la mkesha kata ya Maganzo wilayani Kishapu.
  Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akizungumza na wananchi katika eneo la mkesha kata ya Maganzo wilayani Kishapu.
 Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour akizungumza na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafuta Kishapu.

No comments: