Sunday, July 9, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017: WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, DKT. PHILIP MPANGO AJIUNGA NA PSPF KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI NA KUHIMIZA WANANCHI KUFANYA HIVYO ILI KUFAIDIKA NA BIMA YA AFYA


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (kulia), akikabidhiwa kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, muda mfupi baada ya Mhe. Waziri kujiunga na Mpango huo leo Julai 8, 2017, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ambapo PSPF inatoa huduma zote kwenye Maonesho hayo.
Waziri Dkt. Mpango, (kulia), akimsikilizia kwa makini Bw. Njaidi kuhusu faida zitokanazo na kujiunga na Mpango wa PSS

Waziri Dkt. Mpango(kulia), akipokea fomu ya kujiunga na PSS, kutoka wka Balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msanii maarufu, Mrisho Mpoto. Katikati ni Afisa Habari Mwanamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Habari na Picha wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Rodney Thadeus, akiweka dole gumba kwenye fomu ya kujiunga na uanachama wa PSPF kupitia PSS, leo Julai 8, 2017




NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango,(pichani) amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari na kuhimiza wananchi kufanya hivyo kwani moja ya faida kubwa ni kujihakikishia kuwa na bima ya Afya.

Waziri aliyasema hayo leo Julai 8, 2017, wakati alipotembelea banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasabawakati wa Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea.

“Mimi nitoe wito kwa wananchi kujiunga zaidi na mpango huu kwani watafaidika na huduma ya afya na nyinyi muongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi ili wajiunge zaidi.” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango pia alikabidhiwa kadi yake ya uanachama muda mfupi baada ya kujiunga.

“Mheshimiwa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari una faida nyingi na tumewalenga hasa watu wa kawaida kama vile wajasiriamali, wakulima, mama lishe, bodaboda, na machinga, na tumekuwa tukipata watu wengi wanaokuja kujisajili na Mpango huu na wengi wao wamevutiwa na hii Bima ya Afya ambayo ni moja ya faida azipatazo mwananchama” Alisema Afisa Uhusoano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi wakati akimkabidhi Mhe. Waziri akdi yake ya uanachama.

Bw. Njaidi pia alimwambia Mhe. Waziri kuwa, kwa kujiunga kwake na Mpango huo wa uchangiaji wa Hiari, kutasaidia pia kuwakadia bima ya afya  wasaidizi wake katika miradi kama vile ya shambani na ufugaji.

“ Hawa wote wanawezakuingia kwenye mpango huu wa bima kupitia uanachama wako katika Mfuko.” Alimuhakikishia Mhe. Waziri.

Waziri Mpango (kulia), akiuliza maswali kwa maafisa wa PSPF
Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa za PSPF alipotembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Baada ya Mwanachi huyu kuelewa huduma za PSPF na faida zake kwake, hatimaye alikata shauri la kujiunga na Mpango wa PSS, kwa kujaza fomu kama picha hii inavyojieleza.
Waziri Dkt. Philip Mpango, (kulia), akipokea mkoba wenye vipeperushi vya taarifa mbalimbali za PSPF, kutoka kwa balozi wa Mfuko huo, Msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kutembelea banda la Mfuko huo leo Julai 8, 2017
Mhandisi Ally Shanjirwa wa PSPF, akiwapatia maelezo wananchi hawa waliofika kutembelea banda la Mfuko huo
Bw.Noah Amri, (kulia), Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akizungumza na mwanchi huyu aliyeshika fomu yakujiunga na Mpango huo
Maafisa wa PSPF wakiwa kazini.

No comments: