Mkuu
wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26
ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya
utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro kwa ukarabati
ili yaendane na kazi ya jeshi la p0lisi
Mkuu
wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akijadiliana jamabo na
uongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani
Kilimanjaro wakati alipokagua magari ya polisi yanayofanyiwa ukarabati
mkubwa.
Mkuu
wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akiakizungumza na uongozi wa
Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
Mkuu
wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akikagua moja ya magari 26
ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es salaam yaliyopelekwa katika Garage ya
utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani Kilimanjaro
Mkuu
wa mkoa wa DEar es salaam Mh. Paul Makonda akijadiliana jambo na mmoja
wa viongozi wa Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani
Kilimanjaro.
……………………………………………………………………………
Mkuu
wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo
ametembelea Garage ya utengenezaji wa Magari ya RSA Limited Mkoani
Kilimanjaro kukagua maendeleo ya ukarabati na ubadilishaji mwonekano wa
Magari mabovu 26 ya Jeshi la Polisi yaliyosafirishwa kwenda Moshi Mkoani
Kilimanjaro hivi karibuni.
Akiwa
katika Garage hiyo Mheshimiwa Makonda amejionea magari hayo yakiwa
katika hatua mbalimbali za utengenezaji ambapo ameomba uongozi wa
kampuni hiyo kukamilisha ukarabati wa magari hayo kwa wakati iliyaweze
kuongezea ulinzi na usalama jijini Dar es salaam.
Aidha
Makonda amesema kuwa anataka kubadili mwonekano wa jeshi la polisi Mkoa
wa Dar es salaam kwa kuhakikisha magari ya polisi yanakuwa na hali
nzuri itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa uufanisi kwa
kuyabadili magari hayo kuwa kama yale ya Askari wa umoja wa mataifa.
*”Hakuna
kitu kinachoninyima usingizi kama pale Mwananchi anapohitaji polisi
wafike mahala pa tukio na polisi hawafiki, na kufanya hali ya amani
kutoweka na wakati huohuo polisi wanataka kufanya kazi yao ila
wanashindwa kutokana na uhaba wa vifaa.Hii ndiyo sababu ninahangaika ili
siku moja Dar es Salam iwe na amani hata kufikia hatua ya watu kufanya
Biashara zao masaa 24na kutembea kwa amani muda wote.”*alisema Makonda.
*Nimepata
Pikipiki 200, baiskeli 500 na kuweza kutengeneza magari haya 56 kuwa na
viwango vya kimataifa kama magari ya Umoja wa Mataifa (U.N)
yanavyoonekana,yaani kwenye gari ya doria itaweza kuwa na maafisa wa
polisi tisa kwa nyuma,ambao watatu watakuwa kushoto na watatu kulia mwa
gari hiyo huku wawili wakiwa nyuma ya gari hiyo na mmoja akiwa amesimama
mbele na silaha kubwa.”*aliiongeza Makonda.
Kwa
upande wake kaimu kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam,
(DCP) Lucas Mkondya amempongeza Mheshimiwa Makonda kwa juhudi
anazozifanya kuhakikisha askari wanafanya kizi katika mazingira mazuri.
Nae
mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya RSA Ltd inayokarabati magari hayo
Bwana Varinder Bhamra amesema kuwa watahakikisha ukarabati wa magari
hayo unamalizika kwa wakati huku akieleza kuwa wataendelea kushirikiana
na mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam bega kwa bega.
Ikumbukwe
kuwa Mnamo Mwezi 14 mwaka huu jumla ya magari mabovu ya polisi 26
yalisafirishwa kutoka Dar es salaam kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwaajili
ya kufanyiwa ukarabati na kubadili mwonekano
No comments:
Post a Comment