Monday, June 5, 2017

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi waadhimisha siku ya mazingira kwa kufanya usafi Soko la Mabibo

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wameanzisha siku ya mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la Mabibo sokoni leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho amesema katika uchafuzi wa mazingira sekta ya uchukuzi inachangia kutokana na magari kwa kutoa moshi mchafu.

Amesema katika kuadhimisha siku hiyo kwa sekta ya uchukuzi ni lazima kuchukua hatua katika ulinzi wa mazingira katika vyombo vya moto kafanyia ukaguzi.

Dk. Chamuriho amesema kuwa katika kuendana na sera ya viwanda ni lazima kufanya mazingira kuwa bora ya kuweza kuwavutia wawekezaji mbalimbali .

Aidha amesema kuwa katika maadhimisho ya mwaka huu iwe ni chachu kwa kila mdau wa wa uchukuzi kuwa mtu wa kwanza katika ulinzi wa mazingira.
Nae Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Nchini (NIT), Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa katika maadhimisho hayo wamedhamiria kuwa sehemu mhimu wa kutunza mazingira.

Katika maadhimisho hayo taasisi zilizo chini ya Uchukuzi zimeweza kufanya usafi katika soko la mabibo pamoja na kupanfa miti katika chuo hicho kwa kuungana na shule ya msingi mpakani.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akzingumza katika siku ya maadhimisho ya Mazingira Duniani juu sekta ya uchukuzi kuwa sehemu ya kulinda mazingira.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi ,Mawasiliano na Uchukuzi-Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akipanda mti mti katika chuo cha NIT katika Maadhomisho ya siku ya Mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zakaria Mganilwa akipanda mti katika chuo hicho katika maadhisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo cha NIT, Mombeki Stambuli akipanda mti katika maadhisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Mikoani , Valentine Kadeha akipanda mti katika chuo cha NIT katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wakiwa katika usafi katika soko la mabibo katika mti katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani leo jijini Dar es Salaam.

No comments: