Wednesday, June 21, 2017

WADAU WA SHERIA WATAKIWA KUTOA MAONI KATIKA UTAFITI WA SHERIA YA HAKI JINAI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said akifungua kikao cha Wadau wa sheria mkoa wa Tanga kutoa maoni juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kikao kilichofanyika ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Tanga, kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga akizungumza na Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Anjela Shila ofisini kwake kabla ya kufungua mkutano wa Wadau wa Sheria mkoa wa Tanga.
Mmoja wa wadau akiwasilisha maoni wakati wa Kikao
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Wadau wa sheria mkoa wa Tanga wakimsikiliza Katibu Tawala wa mkoa huo Bi. Zena Said (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kutoa maoni juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kikao kilichofanyika ofisi za Mkuu wa mkoa jijini Tanga.
Baadhi ya washiriki akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Bi. Zena Said wakati wa ufunguzi wa Kikao. (Picha zote na Munir Shemweta -LRCT)



Na Munir Shemweta

Katibu Tawala MkoaTanga Bi. Zena Said amewataka wadau wa sheria kutumia fursa waliyonayo kuchangia kutoa maoni katika utafiti kuhusu taratibu zinazozuia haki jinai.Bi. Said alitoa rai hiyo wakati wa kufungua kikao cha wadau washeria mkoa wa Tanga juu ya utafiti kuhusu taratibu zinazozuia utoaji haki jinai kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Tanga.

Alisema, utoaji maoni yenye tija hususan kwa wadau wa mkoa wa Tanga siyotu utaisadia Tume ya KurekebishaSheria Tanzania katika mapitioya sharia hiyo bali kutaiwezesha nchi kuwa na mfumo wa sheria unaoendana na mabadilikoya jamii.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala mkoa wa Tanga, mfumo wa utoaji haki jinai unakabiliwa na changamoto katika maeneo tofauti yanayohitaji kuangaliwa upya na kwa ukaribu ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na sheria na taratibu zinazotoa haki kwa wananchi kwa wakati na haraka.

Awali Afisa Sheria Mkuu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi. Anjela Shila, aliwaeleza washiriki wa kikao hicho ambao ni Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wilaya, maafisa Upelelezi wa polisi, Wanasheria wa Serikali, Mawakili wa Serikali na wa Kujitegemea , maafisa Magereza na Wanasheria kutoka Asasi za Kiraia zinazotetea haki za Jinai, Tume kwa sasa inaendesha utafiti kuhusu Mfumo wa Sheria ya Haki Jinai juu ya vipengele vinavyozuia haki.

Amevitaja baadhi ya vipengele hivyo kuwa ni pamoja na gwaride la utambuzi, uahirishwaji mashauri mahakamani, haki ya dhamana na mwenendo wakumkabidhi mshitakiwa mahakama kuu.

Bi.Shila alisema, Tume imeamua kufanya utafiti wa haki jinai ili kuangalia changamoto zinazoikabili sheria hiyo na kuzitolea mapendekezo yatakayoboresha mfumo mzima wakutoa haki jinai nchini.

Utafiti wa Mfumo wa Sheria ya Haki Jinai juu ya vipengele vinavyozuia haki unaendeshwa na Tume ya KurekebishaSheria Tanzania katika mikoa yaTanga, Iringa, Mtwara na Morogoro ambapo katika utafiti huo Tume inakutana na wadau wa sheria kwa lengo la kupata maoni ili kuboresha mfumo mzima wa kutoa haki jinai.

No comments: