Mwalimu wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana
kuhusu Nguvu ya Kodi, ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania
(TYVA) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA Taifa Bw.
Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni
“Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman
Makwita akifafanua jambo wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo
leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Muongozaji wa mdahalo huo Bi. Nuria
Mshare na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi.
Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi.
Irene Kalumuna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na
Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare akifafanua jambo
wakati wa mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TYVA,
Bw. Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli mbiu ya mdahalo huo ni
“Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa na
Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakichangia mada wakati wa
mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam
leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana
katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa
na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia mada wakati wa
mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam
leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi wake wa Ushiriki wa Kijana
katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya udhamini wa Shirika la Action Aid.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
No comments:
Post a Comment