Sunday, June 25, 2017

SIMU TV: Habari kutoka televisheni leo

Magari kumi yenye tani 163 za mahindi yaliyokuwa yakizisafirisha kinyume cha sheria kwenda nchini Kenya yamekamatwa mkoani Kilimanjaro. https://youtu.be/HDDgDjIBoKk

Wakulima wa mpunga wilayani Malinyi mkoani Morogoro wamesema kukosekana kwa miundo mbinu bora ya kilimo kumesababisha kutofikia malengo yao. https://youtu.be/NGEZv5bMBA8

Wakazi wa kata ya Lemaoti wilayani Monduli wamelalamika baadhi ya viongozi wasiowaaminifu wanaoshirikiana na wenzao kugawa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo. https://youtu.be/OzCkIrCky5I

Watanzania hapo kesho wataungana na wenzao maeneo mbalimbali duniani kusherekea sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya kuhitimisha mfugo mtukufu wa Ramadhan. https://youtu.be/Zay9Dk_rt3c

Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupita spika Job Ndugai limetoa salamu za sikukuu ya Eid kwa watanzania wote. https://youtu.be/c2zNhneZQCY

Wananwake wa Kiislamu mkoani Kigoma wamefanya maandamano ya kuhitimisha mfungo Mtukufu wa Ramadhan. https://youtu.be/lMs4-oagZfo

Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amemuagiza mganga mkuu wa wilaya ya Mpwapwa kupeleka haraka daktari katika kituo cha afya cha tarafa ya Kibakwe. https://youtu.be/wAZZDwuiL3A

Wadau mbalimbali wa sekta ya afya mkoani Mtwara wametakiwa kushirikiana ili kuweza kupunga vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga. https://youtu.be/Dsq1Iyr-VXQ

Wakazi wa kijiji cha Bolisa wilayani Kondoa mkoani Dodoma wameiomba serikali kumaliza tatizo la maji katika zahanati ya kijiji hicho. https://youtu.be/J2u5D8ekVY4

Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania Dr Fredrick Shoo amewaasa vongozi wa serikali kufanya kazi kwa weledi wakiwa na hofu ya Mungu. https://youtu.be/CbC3RK2nYvw

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars imeanza vyema michuano ya COSAFA huko Afrika Kusini baada ya kuifunga Malawi mabao mawili kwa bila. https://youtu.be/YDfSQ5a0obM

Aliyewahi kuwa makamu wa rais wa shirikisho la soka TFF Athumani Nyamilani ametangaza kujiondoa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Rais wa shirikisho hilo. https://youtu.be/_djIPkGOAS4

Shirikisho la soka duniani FIFA linawachunguza wachezaji wa timu ya taifa ya Russia waliocheza kombe la dunia mwaka 2014 ili kubaini kama walitumia dawa za kusisimua misuli. https://youtu.be/1xJr2Gl6-_Q

Wakati vilabu vya ligi kuu Tanzania vikiwa katika pilika za usajili kwa ajili ya msimu ujao, mambo yaonekana kwenda mrama kwa Ndanda. https://youtu.be/_6qXOE2cEfE

Timu ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono kunako michuano ya COSAFA baada ya kuinyuka Malawi goli 2 kwa 0. https://youtu.be/5cLUdheMRgM

Viongozi wa timu ya Majimaji Fc ya mjini Songea watupiwa lawama baada ya kudaiwa kupora fedha za klabu na kutoka kwa wadhamini. https://youtu.be/Biv-017AEdo

Rais mpya wa chama cha soka Sudan kusini aahidi makubwa katika soka ikiwemo umoja wa kitaifa kupitia michezo. https://youtu.be/7HOBwIlMPLs


Basi la kampuni ya Super Feo lapinduka na kuua mmoja huku wengine wakijeruhiwa wakati likiwa njiani kutoka Mbeya kwenda Songea. https://youtu.be/CgkG6oDpCdI

Wagonjwa katika hospitali ya mkoa wa lindi walalamikia ubovu wa mashine ya X-RAY hospitalini hapo jambo linalopekea adha kwa wagonjwa. https://youtu.be/zDILHh70gy8

Naibu waziri wa nishati na madini awakata wataalamu wa nishati kote nchini kuhakikisha wanawasambazia umeme wananchi waliolipia gharama husika. https://youtu.be/_32UWfl78NA

Umoja wa wabunge kutoka kanda ya ziwa waunga mkono jitihada Rais Magufuli katika kulinda rasilimali za taifa pamoja na utendaji wake. https://youtu.be/sGQTQBVV1aA

Wafanyabiashara waaswa kufanya biashara zao kwa bei ya halali katika kipindi hiki cha sikuu ili kutowaumiza wateja wao. https://youtu.be/KDp5a_d_9ts

No comments: