Asasi isiyo ya Kiserikali ya Marafiki Charity Tanzania ‘Marafiki Charity’, kwa umoja wao jioni ya jana Juni 24. 2017, wamejumuika kwa pamoja katika tukio maalum la kufuturisha katika kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA.
Marafiki hao waliandaa futari hiyo maalum na kwenda kujuika pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha CHAKUWAMA, chenye makazi yake Sinza-Mori (CHAKUWAMA).
Aidha wakitoa shukrani kwa niaba ya Asasi hiyo ya Marafiki Emmanuel Makundi na Omary Mkambara walieleza kuwa, moja ya shughuli waliokuwa wamepanga ni kufanikisha tukio hilo la kujumuika pamoja na watoto hao ikiwa ni njia moja wapo ya kutoa sadaka jamii yenye uhitaji.
“Tumeweza kujumuika hapa kwa pamoja tukiwa Marafiki. Hii ni moja ya kuonesha upendo, undugu, uelewano na hutu wetu kwa wenzetu wa kituo hichi cha CHAKUWAMA.” Alieleza Makundi.
Kwa upande wake, Omari Mkambara alieleza kuwa, huo ni mwanzo kwani wamefurahia uwepo wao hapo wa kupata kufuturu pamoja hivyo ikiemo dua walioombewa ni faraja kwa umoja wao huo.
Marafiki Charity ni muunganiko wa marafiki kutoka kada mbalimbali, waandishi wa Habari, wanasheria, wahandisi, wajasiriamali, wahasibu na watu mbalimbali ambapo wanashirikiana na kwa pamoja katika kusaidia jamii ikiwemo kufanya kazi kwa pamoja za kujitolea, kusaidia wasiojiweza, kubadilishana mawazo na kujumuika pamoja katika mustakabali wa kuijenga Tanzania.
Vijana wa Marafiki Charity wakipeana majukumu kabla ya kuanza jukumu la kufuturisha watoto hao wa CHAKUWAMA.
Ebby mwenye jezi nyeusi akiwatambulisha baadhi ya vijana wenzake wa Marafiki Charity kwa mmoja wa walezi wa kituo cha CHAKUWAMA wakati walipowasili hapo jana Juni 24.2017 katika tukio hilo la kuwafuturisha watoto hao wanaolelewa kituoni hapo.
Baadhi ya wanaumoja wa Marafiki Charity wakiwa kwenye pozi tofauti, akiwemo Devotha, Leah Mushi aliyembeba mtoto Malaika Ebby, Munira Hussen, Esther Namuhisa,na Pendo
Omary Mkambara akijadiliana jambo na Naamala katika tukio hilo la kufuturisha
Wakibadilishana mawazo wakati wakisubiria muda
Omary Mkambara akiwajibika katika tukio hilo
Wakisaidia kushusha futari maalum
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiwa kwenye foleni ya kupata futari hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Shughuli ya futari ikiendelea
Watoto hao wanaolelewa na kituo hicho cha CHAKUWAMA wakiendelea kujumuika pamoja katika furai hiyo maalum iliyoandaliwa na MARAFIKI CHARITY
Marafiki Charity wakiendelea kutoa huduma katika tukio hilo
zoezi la futari likiendelea
Marafiki Charity wakijumuika pamoja katika kupata futari hiyo
Omari Mkambara na Emmanuel Makundi (kulia) wakitoa neno la shukrani kwa kituo hicho
Omary Mkambara akitoa neno la shukrani
Dua maalum kwa ajili ya tukio hilo
Mmoja wa wasimamizi katika kituo hicho akiwatambulisha Marafiki Charity kwa Mama mwanzilishi wa kituo hicho
Marafiki Charity wakimsikiliza Mama Mwanzilishi wa kituo hicho wakati walipofika kumjulia hali
Wakiuliza maswali mbalimbali juu ya kituo hicho cha CHAKUWAMA
Mama Mwanzilishi wa kituo cha CHAKUWAMA akiwaombea dua Marafiki Charity
Baadhi ya Marafiki Charity wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza tukio la kufuturisha watoto wa kituo cha kulea watoto Yatima cha CHAKUWAMA, tukio hilo limefanyika jana Juni 24.2017.
No comments:
Post a Comment