Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (alieshika panga) akikata muwa kuashiria uzinduzi uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa sukari wa Mkulazi wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki.Anaeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kushoto).
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imesema uamuzi uliofanywa na Mifuko ya Hifadhi ya jamii wa kuwekeza kwenye sekta viwanda hapa nchini ni uamuzi sahihi huku ikitoa wito kwa wanachama na wadau wa mifuko kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa zitokanazo na miradi hiyo.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango maalumu wa uwezeshaji wa wakulima wa miwa wa nje (Outgrowers scheme) katika mradi wa Mkulazi iliyofanyika mkoni Morogoro mwishoni mwa wiki chini ya uratibu wa Kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding Ltd ambayo imetokana na na ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage (alieshika panga)akikata muwa kwenye uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kulia).
Mpango huo mpya sehemu ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa na kwa ubia wa mifuko hiyo miwili katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro na unalenga kuwashirikisha wakulima wa (outgrowers scheme)katika kilimo cha miwa kwa kiasi kikubwa ukuanzia na wananchi wa mkoa wa morogoro na Pwani.
“Mbali na kuipongeza mifuko yetu ya Hifadhi ya Jamii kwa uwekezaji huu wenye tija kwa taifa naomba niwasihii sana msikatishwe tamaa na maneno ya watu yanayolenga kupotosha dhana nzima ya uamuzi huu makini lakini nataka niwathibitishie kuwa hadi sasa tupo kwenye mstari sahihi na dalili njema zimeanza kuonekana,’’ alisema.
“Mpango huu licha ya kutengeneza ajira kwa watu zaidi ya 10,000 pia utapunguza na kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa sukari nchini, kuzuia na kupunguza makali ya mfumuko wa bei kwa kuhakikisha bei ya sukari inaendana na gharama za uzalishaji,’’ aliongeza.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe (alieshika panga) akikata muwa kwenye hafla ya uzinduzi huo.Anaeshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage mbali na kuipongeza mifuko hiyo kwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa pia aliongeza kuwa licha ya uwekezaji huo kuhusisha pia kilimo cha mazao mengine ikiwemo mpunga, alizeti, mahindi na mtama pia kuna haja ya kuhakikisha unahusisha uwekezaji katika sekta ya maziwa hoja iliyongwa mkono pia na Waziri Mhagama.
“Pamoja na pongezi zangu ninaomba mradi huu pia uhusishe uzalishaji wa maziwa kwa kuwa tunatarajia kupata mabaki mengi yatokanayo na mazao ambayo yanaweza kugeuka kuwa chakula cha mifugo,’’ alishauri.
Awali wakizungumzia mradi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, walihakikishia serikali, wananchama na wadau wote wa mifuko hiyo kuwa utekelezaji wa mpango huo unahusisha uadilifu na uwazi ili kuleta matokeo chanya.
ZAWADI! Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kushoto) akimkabidhi zawadi Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kwa kutambua mchango wake kwenye mradi huo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe, baadhi ya wabunge wa mkoa wa Morogoro pamoja na muwakilishi kutoka Gereza la Mbigili lililopo mkoani humo.
“Tunajitahidi sana kuzuia kashfa yoyote katika utekelezaji wa mradi huu ili tusiitie doa nia njema ya Mheshimiwa Rais lakini pia kuhakikisha kwamba fedha za wanachama wa NSSF na PPF zinabaki kuwa sehemu salama,’’ alisema Prof Kahyarara.
Akizungumzia mwitikio wa wakulima katika utekelezaji wa mradi huo Bw Erio alisema mwitikio ni mkubwa na hivyo kuwa na uhakika wa malighafi ya kutosha katika kufanikisha lengo kuu la mradi huo unaolenga kuongeza uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili (200,000) zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa hatua ya awali.
Mbali na ujenzi wa kiwanda hicho katika eneo la Mkulazi, uwekezaji huo pia utahusisha ujenzi wa kiwanda kingine cha sukari katika gereza la Mbigili, mradi unaotarajiwa kuzalisha zaidi ya tani 250,000 kwa mwaka, ukichakata miwa isiyopungua tani 2, 500,000 ambazo kwa asilimia kubwa zinatarajiwa kutoka kwa wakulima wa nje kwa lengo la kuongeza ajira.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (wa tatu kulia) akizungumza kwenye hafla hiyo. Wengine ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kushoto) na baadhi ya wabunge wa mkoa wa Morogoro.
TUJIPONGEZE! Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kushoto) ambae kwa pamoja wanatekeleza mradi huo. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio (kulia) akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage katika hafla hiyo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw Charles Mwijage (dereva) na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (abiria) wakijaribu kuhakiki moja ya matreka ya kisasa kwa ajili ya kilimo yanayomilikiwa na Jeshi la Magereza la Mbigiri lililopo mkoani Morogoro walipotembelea gereza hilo kujionea maandalizi ya mradi wa shamba kubwa la sukari pamoja na kiwanda cha sukari kitakachojengwa kwenye gereza hilo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara alipokuwa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na uwekezaji wa shamba la kubwa la miwa katika gereza la Mbigiri.
No comments:
Post a Comment