Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga
wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa
Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na
kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee
Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala
Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack
Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi
mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
Mjasirimalia
Mabela Msolwa kutoka wilayani Kishapu akitoa maelezo kuhusu mradi wake
wa mashine za kuchakata nafaka na ghala kuhifdhi nafaka kwa Mkuu wa mkoa
(kulia) na viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
Mhandisi
wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said (kushoto) akitoa maelezo kuhusu
mradi wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa wananchi kata ya Maganzo.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akitoa maelekezo wakati
alipotembelea ghala la nafaka la Mabela mjini Mhunze kata ya Kishapu
wakati wa ziara yake.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akifafanua jambo kwa
viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo kijiji cha Kinampanda kata ya
Mwamalasa.
Na Robert Hokororo
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika
ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria
uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya
Shagihilu.
Mradi
mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za
mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Kwenye
kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la
kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.
Katika
ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS),
Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa
Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.
Alikaribishwa
na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala
Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa
idara katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment