Mafunzo
hayo ya siku mbili Juni 5 na 6, 2017, yanafanyika katika ukumbi wa
Vigirmark Hotel mjini Shinyanga, na yamekutanisha wadau mbalimbali
wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wizara ya
Elimu, na wakufunzi kutoka mikoa mbalimbali ambako mradi unatekelezwa.
Akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo hayo, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,
Albert Msovela, alisema mfumo wa FFARS utasaidia kwa kiasi kikubwa
katika kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma vinakusanya na
kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi zilizotengwa na Serikali kwa
ajili ya kusaidia maendeleo ya vituo hivyo ili wananchi waweze kupata
huduma bora.
“Ikumbukwe
kuwa Mheshimiwa Rais katika kutekeleza mpango wa elimu bila malipo
aliamuru kuwa fedha za ruzuku za gharama za uendeshaji wa shule lakini
pia vituo vya kutolea huduma zitapelekwa moja kwa moja katika vituo
hivyo, hivyo basi usimamizi wa ruzuku hizo utafanywa na vituo husika,”
alieleza Msovela.
“Lengo
la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo ili kuhakikisha kuwa vituo vyetu
vya kutolea huduma kupitia fedha za ruzuku vinakuwa na mfumo maalum wa
kuandaa taarifa za mapato na matumizi, hali ambayo itachangia
uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” aliongeza Msovela.
Aidha,
alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na PS3 katika
kuunganisha wadau, na kuongeza kuwa ni wakati mzuri watanzania wakaiga
mfano wa nchi kama Marekani ambao wapo mbele zaidi katika masuala ya
uwazi na utawala bora katika kuwapa taarifa wananchi zinazohusu maeneo
yao.
Awali
akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini
na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare, alisema mfumo wa mpya wa
uhasibu na utoaji taarifa - FFARS unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo
ya Kimataifa la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo
ya Sekta za Umma (PS3).
“Tumeandaa
mafunzo ya kina kwa wakufunzi 490 katika ngazi ya taifa na halmashauri,
yatakayofanyika mikoa minne nchini: Dodoma, Mbeya, Mtwara na Shinyanga,
ili kuwawezesha watumishi katika vituo vya afya na elimu kupata ujuzi
wa namna ya kutumia mfumo mpya wa FFARS,” alifafanua Dkt. Kaare.
“Wakufunzi
hawa wataweza kutoa elimu hii kwa watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS
katika zaidi ya vituo vya afya 550, zahanati 6800, hospitali za wilaya
135 na takribani shule za msingi na sekondari 20,000 katika mikoa 26 ya
Tanzania bara, vikiwemo vituo vya kutolea huduma kutoka mikoa 13 na
halmashauri 93 zinazotekeleza mradi wa PS3,” aliongeza Dkt. Kaare.
Katika
hatua nyingine, alisema FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha
zinazotolewa na Serikali katika kufikia malengo ya utoaji huduma na
kuhakisha yanaendana na sheria ya manunuzi na utoaji taarifa, ili
kuisaidia Serikali kuimarisha mfumo wa usimamizi wa fedha za umma na
kuongeza uwazi na watoa huduma kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia.
Naye
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutpka TAMISEMI, Elisa Rwamiago,
alisema mfumo wa FFARS utaanza kutumika kuanzia Julai 1, 2017, ambapo
Serikali itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo
vya afya kwa ngazi za halmashauri.
“Vituo
vya kutolea huduma vitakavyopokea fedha hizo ni pamoja na zahanati,
vituo vya afya, na hospitali za wilaya. Zoezi hili ni sambamba na
inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, serikali za vijiji na ofisi za
kata,” alieleza Rwamiago.
Mwandishi
wetu, Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri wakati wa
mafunzo hayo siku ya kwanza Jumatatu, Juni 5, 2017 .
Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, amefungua mafunzo ya mfumo
mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha
kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System –
FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public
Sector Systems Strengthening – PS3’.
Mgeni
rasmi, Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua
mafunzo kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa
ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and
Reporting System – FFARS) katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini
Shinyanga
Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akifungua mafunzo mafunzo
kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa kwa wakufunzi zaidi ya
130 kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati waliohudhuria mafunzo hayo
Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, akizungumza ukumbini. Kulia
ni Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, na
kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji
kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare
Katibu
Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela, alisema wananchi wana haki ya
kuhoji pale ambapo mambo yanakuwa hayaendi sawa na serikali ina wajibu
wa wananchi inayowatumikia hivyo kuwataka wakufunzi hao kutumia mafunzo
wanayopatiwa kutoa elimu kuwapa pia watu wengine
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza wakati wa ufunguzi
Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji,Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dkt. Suma Kaare akizungumza ukumbini
Afisa
Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, akielezea
kuhusu umuhimu wa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa
ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and
Reporting System – FFARS)
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi TAMISEMI, Elisa Rwamiago, akielezea jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Mshauri
wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma,
Elezeus Rwezaula, akitoa mada wakati wa mafunzo hayo
Mshauri wa Masuala ya Usimamizi wa Fedha za Umma kutoka Mradi wa HPSS Dodoma, Elezeus Rwezaula, akielezea kuhusu mfumo wa FFARS
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Washiriki wa mafunzo wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment