Monday, June 19, 2017

PPF NA NSSF YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA KIKUBWA CHA SUKARI KINACHOJENGWA KATIKA GEREZA LA MBIGIRI

Katika kutekeleza Mradi wa ujenzi wa Viwanda vya sukari Mifuko ya Hifadhi ya jamii NSSF na PPF ilianzisha kampuni tanzu iitwayo Mkulazi ili kuendesha mradi mkubwa wa viwanda viwili vya sukari katika maeneo ya Mkulazi na Mbigiri Mkoani Morogoro.

Mwishoni mwa wiki Bodi ya Wakurugenzi ya Mkulazi ilitembelea moja ya mradi katika eneo la Mbigiri Mkoani Morogoro ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Gadius Kahyarara amesema wametembelea maeneo ambayo ujenzi unaendelea ikiwemo ujenzi wa barabara unaoendelea, ujenzi wa madaraja, na utayarishwaji wa shamba la miwa itakayotumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa PPF William Erio amesema wameshuhudia kazi kubwa inayoendelea ya maandalizi ya shamba na kuridhishwa nayo. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amebainisha kwamba wanatarajia kuanza upandaji wa miwa siku chache zijazo.

Katika ujenzi unaoendelea baadhi ya vijana wasomi wasio na ajira wameanza kujitokeza katika ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkoani Morogoro ili kuunga mkono jitihada za Rais wa awamu ya tano ya Ujenzi wa viwanda.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni tanzu ya Mkulazi inayoundwa na Mifuko ya PPF na NSSF wameridhishwa na jitihda zinazoendelea za ujenzi wa kiwanda baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazoendelea.
Meneja wa shamba la miwa la Mbigiri Prosper Kombe akitoa maelezo kwa Viongozi wa PPF na NSSF kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mku wa NSSF Profesa Gadius Kahyarara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi Holding Company, Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio pamoja na baadhi ya viongozi wa NSSF.
Mjumbe wa Bodi ya Mkulazi Holding Company Martin Mmari ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF akifyatua tofali kwa ajili ya ukarabati wa kiwanda cha sukari Mbigiri.
Meneja Manunuzi wa NSSF Kirondera Nyabuyenze akifyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri.
Shughuli za kilimo zikiendelea katika shamba la miwa la Mbigiri Morogoro.
Ujenzi wa barabara ya kiwanda kipya ukiendelea.
Eneo la shamba linalotarajiwa kuanza upandwaji wa miwa kwaajili ya kiwanda cha sukari Mbigiri Morogoro.
Barabara kuu ya kuingilia kiwanda cha sukari cha Mbigiri ikiwa katika matengenezo.
Baadhi ya vijana wakifyatua tofali kwaajili ya ujenzi wa kiwanda cha Mbigiri Morogoro.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mkulazi Holding Company kushoto Steven Alfred ambaye pia ni Mkurugenzi wa uwekezaji PPF Meneja Uhusiano Lulu Mengele, mjumbe wa Bodi Uphoo Swai ambaye pia ni Mkurugenzi wa Majanga PPF pamoja na Rose Makombe ambae ni mjumbe wa Bodi na afisa sheria wa NSSF.
Jengo la kiwanda cha zamani cha sukari eneo la Mbigiri, ambapo jengo hili litakarabatiwa na kutumika kama ghala la sukari itakayozalishwa na kiwanda kipya.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa daraja katika shamba la Mbigiri Morogoro.

No comments: