Thursday, June 1, 2017

NGULI WA EVERTON LEON OSMAN AZINDUA PROGRAMU YA SOKA LA VIJANA LEO JIJINI DAR.

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.


Mchezaji wa Zamani wa timu ya Everton ya Nchini Uingereza Leon Osman azindua programu ya timu za vijana nchini itakayosimamiwa na timu hiyo uzinduzi uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.

Osman aliyekuwa ameambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe walizindua programu hiyo kwa vijana wadogo ambapo itakuwa endelevu hapa nchini.

Akizungumza na watoto kutoka katika vituo mbalimbali vya kukuzia vipaji vya soka Osman amewataka kujituma zaidi ili waweze kufikia malengo yao.


Osman amewapatia zawadi ya mipira  vijana hao waliokuja na kuonyeshwa kufurahia namna wanavyojituma na kuonyesha vipaji vyao.

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zaman wa Everton Leon Osman (wa pili kulia) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman (anayewasalimia vijana ) sambamba na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone leo Jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa uwanjani na baadhi ya vijana akiwapa maelekezo mbalimbali.
 Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman  akitoa zawadi ya mipira kwa vijana waliojitokeza katika uzinduzi wa programu hiyo itakayokuw aendelelevu chini ya Timu ya Everton.

Mchezaji wa zamani wa Everton Leon Osman akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka vituo mbalimbali pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone.

Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe akiwa na mchezaji wa zaman wa Everton leon Osman (wa kwanza kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara Yusuph Singo (kulia) na Mkurugenzi wa Timu ya Everton Robert Elstone (wanne kulia) na Mkurugenzi wa SportPesa Pavel Slavkov na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Sportpesa Tanzani Abbas Tarimba.

No comments: