Monday, June 19, 2017

MASAUNI ADHAMINI MASHINDANO MAKUBWA YA KUHIFADHI QUR-AN, ZANZIBAR NA TANZANIA BARA


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Diwani wa Wadi ya Kikwajuni, Ibrahim Ngasa wakati alipokuwa anawasili katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge, Unguja, Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika jimbo lake la Kikwajuni yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za jimboni mwake pamoja na maeneo mbalimbali yaZanzibar na Tanzania Bara.Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood (kushoto) akimsalimia Mwenyekiti wa Taasisi ya TAYI, Abdalla Miraji, wakati kiongozi huyo alipokuwa anawasili katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge, Unguja, Zanzibar leo kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara.Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. 

Mwanafunzi Khamis Mussaakionyesha jitihada zake katika Mashindano ya kuhifadhi Qur-an katika Jimbo la Kikwajuni, Unguja, Zanzibar, linaloongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, na mdhamini wa mashindano hayo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani). Mashindano hayo yalishirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara. 
Mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood akimkabidhi zawadi mshindi wa maswali ya papo kwa papo, Ilham Idrisa (kulia). Kushoto ni Mdhamini ya  mashindano hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Watatu kushoto,  Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera. Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauniakizungumza kabla ya mgeni rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood(katikati) kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.Mashindano hayo yaliyoshirikisha Madrasa mbalimbali za Jimbo la Kikwajuni pamoja na maeneo mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara, yalifanyika katika Viwanja vya Mnara wa Kisonge mjini Unguja na kudhaminiwa na Mbunge wa Jimbo hilo. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera 
Sehemu ya washiriki katikaMashindano ya Kuhifadhi Qur-an wakimsikiliza mdhamini wa Mashindano hayoNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati nalipokua akitoa hotuba yake. Katika hotuba yake Masauni alisema washiriki wameonyesha uwezo mkubwa wa kuhifadhi Qur-an.

No comments: