Wednesday, June 14, 2017

MAKINDA AWATAKA WANAWAKE LA BARA LA AFRIKA KUWA IMARA


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mtanzania ,Anna Makinda amewataka wanawake wa bara la Afrika kusimama imara ili waweze kuwa viongozi makini katika kupambana siasa kandamizi kwa Wanawake katika bara la Afrika.

Makinda amesema kuwa zaidi ya miongo kumi imetajwa kuwa huenda mwanamke wa kiafrika akapata ukombozi katika siasa za bara hili,ambazo zinatazamwa kuwa na mlengo wa mfumo dume tangu kuondoka kwa wakoloni .

Aidha hayo yamebainishwa katika mjadala wa kigoda cha Mwalimu unaofanyika kila mwaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali,na kuongeza kuwa siasa za Africa bado zinawagawa wanawake katika mlengo wa kisiasa na kijamii.

"harakati na mambo mengi yamefanyika ili kumkomboa mwananmke wa Afrika na mfumo dume,lakini yote haya yanaonekana kutofanikiwa kwa asilimia miamoja na changamoto ikionekana kuwapo kwa wanawake wenyewe kwa kutothaminiana"amesema Makinda.

Anna makinda amekuwa kiongozi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu iliopita,  anatazama changamoto hii kwa wasichana wa sasa kuwa ni kubwa sana kutokana na mazingira yanayowazunguka .
Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akizungumza katika mkutano wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo mada ya Nafasi ya Wanawake na Siasa za vyama vingi katika bara la afrika iliwasilishwa na wanawake mbalimbali viongozi.
Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mary Nagu akizungumza wakati wa kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam ambapo mada ya nafasi ya Wanawake katika uongozi bara la afrika iliwasilishwa.
Mbunge wa Bunge la Uganda Miria Matembe, akizungumza wakati wa Kigoda cha Mwalimu juu ya nafasi ya Wanawake katika Siasa za Afrika 
Sehemu ya Washiriki waliofika kusikiliza kigoda Cha Mwalimu juu ya nafsi ya Mwanamke katika Siasa za bara la Afrika
Muongozaji wa Mdhalo wa Kigoda cha Mwalimu juu y Mada ya Nafasi ya Wanawake katika siasa za bara la Afrika,Mary Rusimbi akizungumza katika kongamano hilo.
Sehemu ya Washiriki wa Kigoda cha Mwalimu katika ukumbi wa Nkurumah chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa kitivo Cha Sheria Chuo kikuu cha Dar es Salaam,Edda Gideon akichangia mada katika kongamano la kigoda cha mwalimu
Mmoja wa washiriki akichangia mada katika kigoda hicho cha Mwalimu Nyerere
Mwanasiasa Mkongwe , Anna Abdalah akichangia mada katika kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere juu ya nafasi ya wanawake katika Siasa za bara la Afrika
Profesa ,Ruth Meena akichangia jambo katika Kigoda cha Mwalimu juu ya mada ya nafasi ya Wanawake katika siasa za bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Tasisi ya Jinsia katika kigoda cha Mwalimu Nyerere, Dk Eugenia Kafanabo akiongea wakati wa kufunga mjadala wa kigoda cha Mwalimu
Viongozi wa Meza kuu katika mjadala wakiwa katika picha ya Pamoja

No comments: