Wednesday, June 14, 2017

BREAKING NYUZZZZ....: Rais Dkt. Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick ya Canada Profesa John L. Thorton Ikulu jijini Dar es salaam. Katika mkutano huo, uliohudhuriwa pia na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Paramagamba Kabudi na Balozi wa Canada hapa nchini, Ian Myles umemalizika kwa mafanikio makubwa ambapo pande zote zimekubaliana kukaa meza moja kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali katika sekta ya madini. Habari kamili yaja punde


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kulia ni balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Mhe Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa palamagamba kabudi akipeana mikono na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi
Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton akiongea na wanahabari baada ya mazungumzo na rais Dkt Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada (kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kulia ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Canada nchini Mhe Ian wakiwa na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Kushoto ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba kabudi baada ya mazungumzo na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. wakiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles 
Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles akiongea na wanahabari baada ya mazungumzo baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation ya Canada Profesa John L. Thornton baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2017. Pamoja nao ni Balozi wa Canada nchini Mhe. Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi

PICHA ZOTE NA IKULU

No comments: