Monday, June 5, 2017

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA TARIME

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua kiwanda cha kutengenezea Chaki cha Arwa kilichopo Tarime.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime  mkoani Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 
 





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi waache tabia ya kuhujumu miradi ya maendeleo ikiwemo ya wawekezaji kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wilayani Tarime mkoani Mara wakati akikagua miradi ya maendeleo, kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha chaki,kutembea eneo litakalojengwa kiwanda cha sukari na kwenye mkutano wa hadhara kijijini Biswari wilayani humo katika ziara yake ya kikazi ya siku Tatu mkoani Mara.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tabia ya wananchi kupinga kila kitu hata uwekezaji haifai hata kidogo kwani inachangia kuzorotesha shughuli za maendeleo hivyo ni lazima ikomeshwe.

Amewataka wananchi kote nchini washirikiane na Serikali pamoja na wawekezaji wanaokuja nchini kuja kuwekeza kwani kufanya hivyo taifa litapata mapato na wananchi watapata ajira kwenye viwanda vitakavyojengwa nchini.

Akihutubia wananchi wa kijiji cha Biswari katika mkutano wa hadhara, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono kauli ya wananchi wa Tarime ya kutaka kuharakishwa kwa ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika Bonde la Mto na kusema uwekezaji huo utaongeza maradufu mapato ya halmashauri ya Tarime na kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa mkoa huo.

Amesema ataiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuharakisha mchakato wa kutoa vibali ili shughuli za kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda hicho cha miwa kujengwa haraka na kuanza kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Wawekezaji hao kutoka nchini Uganda wanataka kujenga kiwanda sukari kitakachogharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 200 na kuanzisha kilimo cha miwa kwenye eneo la ekari zaidi ya elfu 30 katika bonde la Mto wilayani Tarime.

Kuhusu kilimo cha bangi wilayani Tarime, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza wote wakaze kamba katika kupambana na kilimo hicho ili kikomeshwe wilayani huo.

Amesisitiza viongozi katika ngazi zote na wananchi kwa ujumla washirikiane katika kukomesha kilimo hicho ambacho kimekithiri wilayani Tarime.

Kuhusu Kero ya maji wilayani Tarime, Makamu wa Rais amesema Serikali inatambua tatizo hilo na itafanya kila inavyowezekana ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi wa wilaya ya Tarime.

Amesema Serikali imejipanga vyema katika kuhakikisha tatizo la maji linakuwa historia nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za kiuchumi ipasavyo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji. Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa amemhakikishiwa Makamu wa Rais kuwa Serikali ya mkoa huo imejipanga vyema ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii kwa wakati pamoja na kuimarisha hali ya ulinzi usalama kwa wananchi mkoani humo.

No comments: