Wednesday, June 14, 2017

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro azoa Milioni 20 za Biko


Balozi wa Biko Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, wakihakiki namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Sinyangwa na kumpigia ili kumjulisha juu ya ushindi wake.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MOTO wa bahati nasibu ya Biko ama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, umezidi kuchanja mbuga baada ya droo yake ya 14 kufanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Kilosa Morogoro, Magreth Sinyangwa, akiwa mwanamke wa kwanza kuzoa jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini.

Droo hiyo iliyompelekea utajiri mshindi huyo wa Morogoro, imechezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja na kushuhudiwa pia na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiagana na mwakilishi wa Bodi Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humud Abdulhussein, mara baada ya kumaliza kuchezesha droo ya 14 ya Sh Milioni 20 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam, huku Magreth Sinyangwa akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na mamilioni hayo ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo hususan kwa droo kubwa za Sh Milioni 10 hadi 20.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema moto wa Biko umezidi kuchanja mbuga baada ya kumpata mshindi wao wa Sh Milioni 20, huku kwa mara ya kwanza wakimpata mshindi ambaye ni mwanamke tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.

Alisema washindi hao ni wale wanaocheza bahati nasibu yao kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money, ambapo watatakiwa kuingia kwenye lipa bili au lipa kwa M-Pesa na kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya kumbukumbu 2456 tayari kwa kucheza.

“Baada ya kuingiza namba ya kumbukumbu pia atatakiwa kuweka kiasi cha kucheza ambacho kinaanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo kiasi cha Sh 1000 kitampatia nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 kwa Jumapili ijayo kama tulivyompata mwingine kwa droo tuliyochezesha jana.

“Kwa zawadi za papo kwa hapo zinaanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo mshindi hutumiwa fedha zake dakika chache baada ya kupokea ujumbe wa Biko ukimtaarifu juu ya ushindi wake kutokana na kucheza Bahati Nasibu yetu,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili waweze kujiwekea mazingira mazuri ya kuibuka na zawadi mbalimbali za Biko.

Naye mshindi huyo Magreth Sinyangwa akizungumza kwa simu baada ya kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 alisema hakuamini kama ameshinda kiasi hicho cha pesa baada ya kujulishwa hivyo na Kajala, huku akisema kuwa amepokea kwa furaha kwa sababu zitamkwamua katika shughuli zake za ujasiriamali.

“Nashukuru Biko kwa kunijulisha juu ya ushindi wangu mnono wa Sh Milioni 20 ambazo kwa hakika zimekuja wakati muafaka kwa sababu tayari nimepata kitu cha kuniletea utajiri mkubwa kutokana na kushinda kwangu donge nono la Biko kama waliyokuwa wanashinda wengine,” Alisema Magreth.

Naye Humud Abdulhussein ambaye ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, alisema mchezo wa Biko unafuata kanuni, sheria na taratibu zote zilizowekwa na serikali kwa kusimamiwa vizuri na Bodi yao ili kuhakikisha michezo ya kubahatisha inakuwa salama.

Bahati Nasibu ya Biko imekuwa ikizidi kutoa washindi wengi wa papo kwa hapo na wale wanaoshinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 10 hadi 20, huku jumla ya Sh Milioni 500 zikitolewa kwa mwezi Mei pekee, jambo linaloashiria mafanikio makubwa kwa wanaoshiriki mchezo huo wa Biko.

No comments: