Sunday, June 18, 2017

FUTARI YA KARIAKOO FAMILY DEVELOPMENT FOUNDATION (KFDF) 2017

TAMKO LA SHUKURANI
Kwa niaba ya uongozi wa KFDF, napenda kuwashukuru watu wote waliotoa michango mbali mbali  kufanikisha shughuli yetu ya leo ya kufuturisha. Shukrani za kipekee zimwendee Mwenyekiti wetu Alkarim Bhanji, Makamu mwenyekiti, Mohammed Irapo, Mweka Hazina Msaidizi , Bakari Simba na Iddi Abdallah kwa uwajibikaji wao uliopelekea kufanikisha shughuli mpaka dakika ya mwisho ya kukunja majamvi.
Uongozi una deni kubwa kwa watu wote waliojinyima na kutoa michango ya ziada ili kuziba mapengo ya gharama tulizokabiliana nazo. Pia kuna ndugu zetu wengine waliojitolea kutoa misaada ya bidhaa za chakula kwa ajili ya kuwapa watoto yatima. Bidhaa hizo ,vikiwemo , Ngano ,Mchele, Sembe na nguo. Bidhaa nyengine za Msaada kwa watoto zilinunuliwa kutoka kwenye pesa tulizochanga . baadhi ya bidhaa hizo ni Mchele, Sabuni, Sukari na Juice. Kwa upande mwengine ; pesa zilizobaki baada ya kununua hizo bidhaa walipewa wakuu wa vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kusaidia matumizi mengine hapo kwenye vituo vyao.
Pia nawashukuru wana kariakoo wote wa KFDF na KFG waliojitokeza kuhudhuria hafla hii.
Vile vile kwenye Shughuli hii palihudhuriwa na Masheikh wa Kariakoo,  wajumbe kutoka Gogo vivu, wajumbe kutoka kalabu ya Saigoni na watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo viwili tofauti. Kituo cha Madina kilichopo Tandale na Kituo cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani.
Nakushukuruni wote. Na bila ya shaka mtayapata malipo yenu ya ukarimu  wenu kutoka kwa mola. Allah akituwezesha kufika salama mwakani, tutaweza kuwa pamoja na vituo vya watoto yatima zaidi ya hivi tulivyokuwa navyo leo.
Ahsanteni Sana,
Katibu Mkuu KFDF
Waheed Abdul.

 Kisomo wakati wa hafla ya futari ya Kariakoo Family Development Foundation iliyofanyika jana mtaa wa Tandamti na Livingstone na kuhudhiriwa na wanachama, masheikh wa Kariakoo na viongozi wa Saigon Sports Club 
  Kisomo wakati wa hafla ya futari ya Kariakoo Family Development Foundation iliyofanyika jana mtaa wa Tandamti na Livingstone na kuhudhiriwa na wanachama, masheikh wa Kariakoo, viongozi wa Saigon Sports Club, wajumbe kutoka Gogo vivu pamoja na watoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani 
 Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
 Picha ya pamoja ya wanachama wa KFDF na watoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
 Picha ya pamoja ya badhi ya wanachama wa KFDF
  Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
  Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
  Misaada ilitolewa kwawatoto wanaolelewa kwenye vituo viwili vya Yatima vya Madina cha Tandale na cha Maalim Bonge kilichopo Jangwani
 Picha ya pamoja ya baadhi ya wanachama wa KFDF
 Picha ya pamoja ya baadhi ya wanachama wa KFDF
 Misaada ikiandaliwa kabla ya kugawiwa
 Baadhi ya wanachama wa KFDF katika hafla hiyo
 Baadhi ya wanachama wa KFDF katika hafla hiyo
 Baadhi ya wanachama wa KFDF katika hafla hiyo
 Wanachama wa KFDF na watoto yatima katika hafla hiyo
 Baadhi ya wanachama wa KFDF katika hafla hiyo
Wanachama wa KFDF na watoto yatima katika hafla hiyo

No comments: