Tafadhali pokea CODES hapa chini
Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa
watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza,
Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati ambayo itatumika
katika halmashauri za mikoa hiyo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa,
John Mongela alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani
yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza
mipango mikakati katika maeneo yao.
Alisema kwa dhamana waliyonayo watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo
hayo ya siku mbili vizuri ili baada ya mafunzo waweze kupata njia
mbadala katika uandaaji wa mipango mikakati ambayo itasaidia kuleta
maendeleo Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi
wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa
Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa
Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati
“Hampo
hapa kwa ajali, mpo kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia
mafunzo haya mtapata nyezo za kupangia mikakati ya kweli na mimi
nataraji mtatoka hapa vizuri, haya ni mafunzo muhimu sana,
“Tusiishie kwenye mikakati, tatizo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi,
tumekuwa na mawazo mengi sana lakini tuna changamoto ya kuyaweka kwenye
miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo na sasa tuanze kuyafanyia kazi,”
alisema Mongela.
Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka
washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na ESRF kwani tayari wameonyesha
nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha mipango ambayo wanaipanga
inafanyiwa kazi. Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za
Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango
wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu
uandaaji wa mipango mikakati.
“Tuone
jinsi gani tunatumia fursa hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa
tukatekeleze mipango hii na ESRF wapo tayari kushikana mikono na sisi
hadi waoane mafanikio na mimi niwahakikishie sisi tupo tayari …
nategemea mambo makubwa baada ya kuanzisha ushirikiano huu,” alisema
Mheshimiwa Mongela.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi
kirefu wamekuwa mstali wa mbele kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu
kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF
imekuwa ikisimamia na kuhimiza ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika
ngazi ya Taifa bali pia katika ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema
Dk. Kida Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela (katikati) akizindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya.
Dk.
Kida aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo kutakuwa na mada zinazoelezea
maelezo ya Jumla kuhusu mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji
na namna ya kutoa taarifa, mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa
SDGs, FYDP II, Africa Agenda 2063, Vision 2025, mchakato wa kuandaa
mpango mkakati na ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting,
monitoring and evaluation)
Aidha ESRF imezindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya,
mwongozo ambao umetokana na andiko kubwa lililoandaliwa na serikali siku
za nyuma kuhusu uandaaji wa mipango mkakati ya muda wa kati pamoja na
bajeti (Government’s Medium Term Strategic Planning and Budgeting
Manual).
Meza kuu ikionyesha mwongozo huo baada ya kuzinduliwa rasmi. Bwana Apolinary Tamayamali kutoka Ofisi ya Rais-IKULU akitoa neno kwa washiriki kuhusu mipango na mchakato wa uandaaji bajeti. Picha
juu na chini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Self Microfinance Fund, Mudith
Cheyo akitoa mada kwa washiriki kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.[/caption]
Picha
juu na chini ni Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mipango mikakati
ambayo yamehusisha watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa
Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa
Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu.
Picha
juu na chini ni Washiriki wa mafunzo kuhusu uandaaji wa mipango
mikakati wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mheshimiwa, John Mongela.
No comments:
Post a Comment