Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Balozi, Dismas Assenga.
Raisi wa Jumuiya ya watanzania waishio Houston Marekani Bw. Daudi Mayocha (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mijini Houston.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (aliyesimama, wapilikushoto) akitoa maelekezo ya jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki ya KCB kwa baadhi ya watanzania (pichani) wanaoishi katika mji wa Houston.
Raisi wa jumuiya ya watanzania waishio Dallas Marekani Bw. Ben Kazora (kushoto) akimshukuru Meneja Mahusiano wahuduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi Shose Kombe (kushoto) kwa kuwapelekea huduma za kibenki mjini Dallas.
Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Bi. Shose Kombe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaoishi katika mji wa Dallas.
Benki
ya KCB Tanzania kupitia dawati lake la Diaspora Banking inafanya ziara
katika miji waishio watanzania nchini Marekani. Ziara hii imeanza tarehe
26 Mei na kutegemewa kumalizika tarehe 7 Juni. Miji inayotembelewa ni
Washington Dc, Houston, Tx, Dallas, Durham Raleigh, Nc Boston, Ohio,
Minnesota Na Chicago.
Meneja
Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje ya Nchi,
Bi. Shose Kombe akizungumza kuhusiana na ziara hii, alisema “Kuna
watanzania wengi wanaoishi nje ya nchi na wanahitaji kuwekeza na kupata
huduma za kibenki nyumbani wakiwa mbali na Tanzania, hivyo Benki ya KCB
inatembelea miji ya Marekani yenye watanzania wengi ili kuwapatia huduma
bora kwa haraka, usalama na bila usumbufu”.
Huduma
za kibenki wanazopatiwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni; akaunti za
akiba (savings), akaunti za uwekezaji (Investment), akaunti za
wanafunzi, akaunti za watoto na fursa ya kununua nyumba (Mortgage) kwa
lengo la kuwawezesha watanzania hao kuendesha shughuli zao za kibenki
Tanzania huku wakiwa nje ya nchi na kupata akiba zao pindi watakapo rudi
nchini Tanzania.
“Huduma
hizi za kibenki kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi ni za papo kwa
hapo (real time transactions), hivyo kuwawezesha wateja wake kufanya
mambo kwa wakati na bila kadhia popote pale walipo duniani” alisema Bi.
Kombe.
Akizungumza
na Meneja Mahusiano wa huduma za kibenki kwa Watanzania wanaoishi nje
ya Nchi, Bi. Kombe na watanzania wanaofanya kazi ubalozini, Kaimu Balozi
wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Dismas Assenga alifuraia ujio wa
benki ya KCB nchini Marekani.
“Watanzania
wanaoishi Marekani wanahitaji sana kuwekeza nyumbani hivyo tutafurahi
mkifikia watanzania wote kutoka miji tofauti ya Marekani” alisema Kaimu
Balozi. Bi. Kombe alimaliza kwa kuwataka watanzania wanaoishi nje ya
nchi na bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo, mteja anahitaji
kua na nakala ya Pasi ya kusafiria, Leseni ya udereva au risiti ya
huduma za umeme au maji (utility bills).
No comments:
Post a Comment