Wednesday, May 17, 2017

WADAU WA ELIMU TANZANIA WAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE - HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII KUWASILISHA MAPENDEKEZO YA ELIMU

Picha ya pamoja ya wadau wa elimu Tanzania na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge, huduma na Maendeleo ya Jamii baada ya kikao cha kuwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka wa fedha 2017/2018 uliofanyika katika ukumbi mdogo wa bunge mjini Dodoma.

Baada ya Kikao hicho wanakamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii waliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa elimu ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii, Mhe. Azzan Zungu akifungua kikao na kuwakaribisha wadau wa elimu waliofika katika mkutano huo ili kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18.
Kiongozi wa wadau wa elimu Tanzania(Head of Deligation) , Ndugu Saddam Khalfan akielezea madhumini ya kikao hicho kilichokuwa kinahusiha kuwasilisha mapendekezo na maoniya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18 kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.
Mwakilishi wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Ndugu Karoli Kadeghe kutoka ACTIONAID Tanzania akiwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu kuhusu serikali kuongeza uwekezaji wa fedha za ugharamiaji elimu kupitia rasilimali za ndani ili kuepukana na utegemezi wa fedha za wahisani kwa wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.

Pia aligusia umuhimu wa uwekezaji wa miundombinu ya shule na kuboresha maslahi ya walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Katibu mtendaji wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania, Ndugu Alphonce Lusako akihimiza na kuishauri kamati ya bunge kuisimamia serikali kutoa bajeti ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wote wenye sifa wanaodahiliwa vyuo vikuu nchini bila ubaguzi wowote. Bajeti husika ijikite katika maboresho ya mafunzo kwa vitendo kazi (Internship), mafunzo ya ufundi stadi na kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Pia aliiomba kamati hiyo kutoa pendekezo kwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo kuweka utaratibu thabiti na endelevu wa Kukusanya fedha za mikopo kwa wanufaika waliokwisha nufaika na mikopo hiyo ilikuongeza Wigo wa kuwapa mikopo wanafunzi wapya wa vyuo vikuu nchini. 

Pia tunaiomba serekali Ilitazame upya suala la ukusanyaji wa madeni ya walionufaika na mikopo, kubadilisha ghafla Makusanyo toka asilimia nane (8%) hadi asilimia kumi na tano(15%) ni kuvunja mkataba wa mkopaji na mkopeshaji, jambo hili linavunja sharia. Kama ni lazima kufanya hivyo basi makusanyo hayo ya asilimia kumi na tano (15%) yaanzie kwa hawa wanaokopeshwa sasa ili wakope wakiwa wanalijua hilo.
Baadhi ya wanachama wa Mtandao wa elimu Tanzania(Ten Met) wakichangia mada kuhusu bajeti ya elimu katika masuala kama kuruhusu wanafunzi waliopata ujauzito kurudi mashuleni, upungufu wa madarasa pamoja na vitendea kazi vya elimu.
Wajumbe wakiangalia video ya hali halisi ya baadhi ya shule nchini pamoja na makazi ya walimu iliyoandaliwa na ActionAid Tanzania na Ten Met.

No comments: