Friday, May 19, 2017

STAR TIMES YAINGIA UBIA NA TPB KUUZA LUNINGA ZA KIDIJITALI KWA MKOPO

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akikata utepe kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mikopo ya Luninga za kisasa kwa kushirikiana na Star Times.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal wakifungua kitambaa kwa pamoja na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya kuashiria uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akipeana Mikono na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya mara baada ya uzinduzi wa huduma za mikopo ya Luninga za Star Times Kupitia benki ya Posta.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal na Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya wakionyesha moja ya Luninga zitakazokuwa zinakopeshwa kupitia benki ya Posta.
Baadhi ya watumishi wa kampuni ya StarTimes Tanzania ambao wamehudhuria sherehe hiyo
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal akizungumza mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo ya ukopaji wa Televisheni za Star Times.
Meneja wa Teknolojia wa Benki ya Posta Tanzania(TPB), James Msuya akizungumzia namna ya kuapata mkopo kutoka benki hiyo
Sehemu ya Watumishi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika Duka la Star Times Bamaga




Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kampuni ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.

akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mpnago huo Makamu wa Rais wa Star Media Tanzania Zuhra Hanif Fazal, amesema kuwa ubia huo unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB.

"wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo" amesema Zuhra.

Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi amesema ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes.

Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.

“Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia”

Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. 

Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.

Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
Meneja Mahusiano wa StarTimes, Antony Katunzi akizungumza na namna ya kutumia Luninga hiyo iliyo na king'amuzi ndani
Meneja Masoko wa Benki ya TPB,Amos Kisanga Akizungumza juu ya watu kufungua akaunti benki ya Posta na kuweza kukopa Luninga. 

No comments: