Monday, May 29, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli leo amewatembele na kuwajulia hali wagonjwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. https://youtu.be/qzmI8Z7m7Gg

SIMU.TV: Mwenge wa uhuru umendelea na mbio zake jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Kigamboni na kuzindua mradi wa barabara inayoanzia kwenye daraja la Kigamboni hadi kwa Msomali. https://youtu.be/9lRKbnDF1r0

SIMU.TV: Wananchi zaidi ya elfu moja walijitokeza katika upimaji wa maambukizi ya VVU katika mbio za mwenge mkoa wa Lindi ambapo kati yao wananchi 20 waligundulika kuwa na maambukizi virusi vya UKIMWI. https://youtu.be/DeMdNfAnbCQ

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira Januari Makamba amesema ekari 2500 za misitu zinateketezwa kila siku nchini jambo linalotishia kusababisha jangwa. https://youtu.be/dkXqIWd5PhA

SIMU.TV: Wakulima wa zao la mahindi katika wilaya ya Mbozi wameaswa kuacha kuuza mahindi ghafi badala yake wasage unga na kuuza ili kuongeza thamani. https://youtu.be/3YNRXJYos7w

SIMU.TV: Serikali ya Tanzania kupitia chuo cha utumishi wa umma kimeisaidia serikali ya jimbo la Putland kuboresha sekta yake ya utumishi wa umma kwa kuendesha mafunzo kwa watumishi wa jimbo hilo. https://youtu.be/WNpp-bFH34A

SIMU.TV: Mauji yanayoendelea katika mkoa wa Pwani yameelezwa kuathiri maisha ya akina mama kutokana na wengi kubaki wajane na watoto kubaki yatima. https://youtu.be/pjIJWjAv5bU

SIMU.TV: Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Temeke wameungana katika kuaga mwili wa Bi Tausi Milanzi aliyekuwa diwani wa kata ya Kijichi. https://youtu.be/-sjCBp4zIeg

SIMU.TV: Nahodha wa klabu ya Simba Jonas Mkude leo amenusurika katika ajali ya gari iliyosababisha kifo cha shabiki mmoja walipokuwa safarini kutokea mkoani Dodoma kurejea Dar es Salaam. https://youtu.be/gwy6xq7ur1Y

SIMU.TV: Timu ya soka ya Lipuli Fc kutoka mkoani Iringa imefungua milango kwa wachezaji wanaotaka kusajiliwa na timu hiyo kwenda kufanya majaribio. https://youtu.be/aUzaS3XIJSM

SIMU.TV: Dereva wa magari ya mwendo kasi wa timu ya Ferrari ameibuka mshindi kwenye michuano ya Monaco mwaka huu baada ya kuwapita wenzake licha ya kuanza michuano hiyo kwa kasi ndogo. https://youtu.be/3hc5-xbIVYg

No comments: