Thursday, May 4, 2017

RAS TANGA ATAKA WAANDISHI WA HABARI KUPEWA USHIRIKIANOKatibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akifungua maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) leo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Msaidizi Alex Abraham

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi mara baada ya kupokea cheti cha kuripoti habari za majanga na hali hatarishi jana mafunzo waliyoyapata mkoani Morogoro hivi karibuni katika halfa iliyofanyika

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George naye akipokea cheti hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Amina Omari naye akipokea cheti hicho

Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na Mwandishi wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea cheti
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea cheti .

Mmiliki wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga,Salum Mohamed naye akipokea cheti hicho

Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press Klabu,Lulu George

Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani Tanga,Frank Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo leo
Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo kulia ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George

Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo
Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF),Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwandishi wa gazeti la Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Klabu)Neema Omary kulia na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo,Amina Omari wakifuatilia matukio mbalimbai

KATIBU Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Said ameziagiza taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye taasisi hizo kwa ajili ya kuhabarisha umma.

Ameyazungumza hayo leo wakati wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa Tanga maazimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya waandishi wa habari kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya taasisi za Serikali kushindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji kutekeleza majuku yao ya kazi.

Burhan Yakubu ambae ni mjumbe na mwaandishi wa habari alisema kumekuwepo na utaratibu usioendana na maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali hiyo

“Tumekuwa tukikwama kutekeleza wajibu wetu hasa tunapohitaji kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo limekuwa liktkwamisha katika shughuli zetu”Alisema Yakubu.

Akitolea ufafanuzi malalamiko hayo Mhandisi Zena alisema taasisi zote zinapaswa kutambua kuwa wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza majukumu yao.

Mhandisi Zena alisema zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka kutekeleza wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Tusiwawekee mipaka waandishi wakati wanapotaka kutekeleza majuku yao na tayari nimekwisha toa agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa taasisi zote,hakuna jambo linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata kwa wakati ikiwa hakuna waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni kubwa kwa Taifa Hili.”Alisema

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili yatakayokuwa na maslahi mapana kwa ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.

Katika hatua nyingine Mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga,Kamishna Msaidiz,Mwandamizi wa Polisi Benedict Wakulyamba,juu ya usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano ya kisiasa.

Mbaruku alisema hivi karibuni kumeripotiwa kutokea matukio kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali hapa nchini kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kushindwa kuwajibika katika harakati zao za kupata habari kwa lengo la kuhabarisha umma na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu ya usala wa maisha yao.

Kamanda wakulya alisema jukumu la usalama lipo mikononi mwa jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua uwepo wa waandishi na umuhimu wao katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa waandishi hao kuziona dalili za uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema kabla ya madhara makubwa hayaja tokea.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: