Thursday, May 4, 2017

Mshindi wa mashindano ya 'Bball Kings' kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 10

 Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe  akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar kuhusiana na zawadi mbalimbali zitakazotolewa katika Mashindano hayo,na pia vigezo vitakavyotumika katika ushiriki wake.
 Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. (kulia),ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo,akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,mapema jana jijini Dar,naona ya kuyaboresha mashindano hayo ambayo yamekuwa yakiwavutia mashabiki wengi wa mchezo huo
Pichani kushoto ni Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda akitoa ufafanuzi kuhusiana na mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.,mbele ya Waandishi wa habari mapema jana,ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kurindima ndani ya mwezi huu wa Mei na kufikia tamati mwezi Julai,mwaka huu.Pichani kati ni Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe na kulia ni Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. 

==== ==== ==== ========
 
Kituo cha East Africa Television (EATV) na East Africa Radio kwa udhamini wa Kinywaji cha Sprite, kiimeandaa mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda alisema kuwa 
yanatarajia kufanyika katika viwanja tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia mwezi huu wa Mei na kufikia tamati mwezi Julai mwaka huu.
 
Kabinda alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali za mpira wa kikapu kutoka pande mbalimbali za Tanzania.

" Dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji vipya katika mchezo wa kikapu hapa nchini.Mashindano haya yamepatiwa kibali kuendeshwa hapa nchini kwa kuzingatia sheria za Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),na kwamba mashindano haya yatakuwa na hatua kuu saba",alisema Mwenze Kabinda.

Kabinda alizitaja hatua hizo saba kuwa ni :-1. Usahili,2. Warsha 3. Kufuzu,4. Kumi na sita bora,5. Robo fainali,6. Nusu fainali 7. Fainali

Nae Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe alizitaja zawadi za mashindano hayo kuwa Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi milioni kumi (10 Milioni) pamoja na kombe la ubingwa wa Bball Kings kwa mwaka 2017. Mshindi wa pili atapata shilingi milioni tatu (3 Milioni). Mchezaji bora wa mashindano atapata shilingi milioni mbili (2 Milioni).

Mbowe alivitaja vigezo vya kushiriki mashindano hayo kuwa ni;  Kwa mwaka huu wa mwanzo, mashindano haya yatajumuisha vijana wa kiume pekee,Watu wataruhusiwa kuunda timu zao za mtaani, kila kikosi kitaruhusiwa kuwa na wachezaji wasiozidi wa 3 kutoka timu za daraja la kwanza,Kwa timu shiriki isipungue wachezaji 10,Timu itaruhusiwa kuwa na -Mshiriki awe na umri usiopungua miaka 16,Mshiriki awe ni raia wa Tanzania.

Katika hatua nyingine Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe amewashukuru kwa dhati wadhamini wao Sprite kwa kuwaunga mkono mkono na kuonesha imani yao kwa kituo hicho cha EATV, pia kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kutoa kibali cha kuendesha mashindano hayo.

No comments: