Friday, May 19, 2017

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA MPOGOLO AWAFUNDA VIONGOZI, WANACHAMA JIMBO LA SEGEREA NA UKONGA


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Tabata, Jimbo la Segerea, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana.
Wanachana wa CCM Jimbo la Segerea wakiinua mikono kufurahia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo,jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wanachama, Viongozi wa CCM Kata ya Pugu, Jimbo la Ukonga wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana. Mkutano huo ulifanyika kwenye Ukumbi wa Check Point, Pugu. 
Wanachama wa CCM Jimbo la Ukonga wamsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogolo,wakati 
akiwahutubia kwenye Ukumbi wa Check Point jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwatambulisha Madiwani wa Jimbo la Segera na kuwapa majukumu wakati wa mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akizungumza jamabo na mmoja wa wanachama wa CCM Kata ya Pugu wakati akiondoka baada ya kymaliza mkutano wake katika Jimbo la Ukonga jana.


***********************************************


Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

UBABE na unafiki wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) inaelezwa kuwa ndio chanzo cha kupoteza jimbo la Ukonga na mengine ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema hayo jana wakati alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama katika majimbo ya Ukonga na Segerea.

Alisema viongozi hao waliendekeza mizengwe na umimi, ambapo matokeo yake waliwavuruga wanachama na jimbo likachukuliwa na upinzani,sasa wanajuta.

"Tumewasababishia wanachama kubaki kama wakiwa, hawana mbunge,na sehemu zingine hawana madiwani. Yote ni kutokana na ubinafsi na makundi yaliyokiumiza Chama,"alisema.

Mpogolo alisema CCM haiwezi kukubali viongozi wachache wenye roho za chuki waendelee kuwanyanyasa wanachama wenzao kwa sababu ya maslahi ya makundi yao."Naomba kila mwanachana afanye mabadiliko ndani ya nafsi yake. Hatuna namna nyingine zaidi ya 

kubadilika na kujenga taswira nzuri ya Chama chetu. Mtu anayeona hawezi kubadilika aende vyama 
vingine," alisema.Aliwataka viongozi na wanachama kuvua makoti ya zamani yaliyojaa chuki,roho mbaya na ubinafsi na badala yake wavae makoti mapya ya upendo ,umoja na mshikamano na kuingia kwenye timu ya ushindi ya CCM mpya na Tanzania mpya.

Akiwa katika jimbo la Segerea, Mpogolo aliwapongeza kwa kushinda jimbo hilo na aliwapa pole kwa kupoteza kata zote za jimbo hilo,lakini aliwataka wajitathmini maana wanajua nani aliyepoteza.Mpogolo alisema chanzo cha kupoteza kata zote 13 ni wana CCM walioamua kuuza kata zote na kuwafanya wananchi wakose 'connection' Mwenyekiti wa Chama Rais Dk. John Magufuli.

"Tumeweka madiwani hawana hata mawasiliano na Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama chetu. Hata kuwaletea maendeleo itakuwa ndoto kwa kuwa hawana 'connection'na baba,"alisema.Aliwataka wanachama kuanza kujiandaa mapema kutafuta wafuasi kwa kujenga uhusiano mwema na kuwa kishawishi kwa wananchi wengine ili kuongeza jeshi la CCM.

"Ili ushinde unahitaji wafuasi wengi na uwe kivutio.Sasa kwa tabia zetu za figisu figisu, hasira makundi, kushughulikiana tutawezaje kuvuta wafuasi.Ndio maana nawataka mbadilike ndani ya nafsi zenu,"alisema.

Akizungumza kwa mifano Mpogolo alisema baadhi ya viongozi wamekuwa vikwazo na kuwakera wanachama mpaka wengine wanakimbia CCM jambo ambalo halina nafasi katika awamu hii."Kama tumejaa chuki, kufukuzana, kuchafuana ,kupakana matope,hatutaweza kuwavutia wanachama wapya. Wanaofitini wenzao na kufukuzana bila sababu za msingi hawana nafasi CCM,"alisema.

Awali Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe,alisema jimbo la Segerea ndio eneo pekee ambalo Chama kilipoteza kata zote na hailezeki ilikuwaje maana mbunge aliyeshinda ni wa CCM Bona Kaluwa.Alimuomba Mpogolo, awafunde wanachama wa CCM waondokane na mapepo yaliyosababisha wauze kata zote za jimbo hilo.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joyce Kaugala ,alisema ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama ,itasaidia kuwajenga wanachama ili uchaguzi ujao waweze kukomboa kata zote.

No comments: