Monday, May 29, 2017

MWENGE WA UHURU WAKAGUA MIRADI MANISPAA YA KIGAMBONI YA SH.BILIONI 229.4

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
 MWENGE wa Uhuru umezunguka katika Wilaya ya Kigamboni na kugagua miradi ya maendeleo saba yenye thamani ya Sh bilioni 229.4
Akizungumza wakati wa kuitimisha Kata ya Kimbiji wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mkuu wa  Wilaya hiyo, Hashimu Mgandilwa,  aliitaja miradi hiyo ikiwa ni pamoja na Barabara inayounganisha daraja la Mwalimu Nyerere na barabara ya Ferry kwa thamani ya Sh.bilioni 21.
Mwenge huo umezindua Chama Cha Kuweka na kukopa cha Tulemune  chenye  mtaji wa Shilingi milioni 25, Mradi wa Ufugaji wa Samaki katika kata ya Kibada wenye thamani ya Shilingi milioni 400.
 Mgandilwa amesema Mwenge wa uhuru umewezesha kuzinduliwa kwa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzindua Jengo la kutolea huduma ya mama na mtoto pamoja na vifaa vya zahanati ya Kisarawe II.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour, aliwataka wananchi kuendelea kuanzisha viwanda ili kufanikisha kampeni ya serikali ya kufikia uchumi wa kati tutakapofikia mwaka 2020.
Amesema kuwa watu hawapaswi kusubiri kupata mitaji mikubwa ndio waanzishe viwanda na kwamba wanapaswa kuanzia katika viwanda vidogo kwani hata nchi zilizoendelea zilianza hivyo.
Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Lake  kinachozalisha saruji ya Nyati, Afroz Ansary aliiomba Serikali kukarabati miundombinu ya barabara ya kuelekea kiwandani hapo kwani imekuwa changamoto kwa biashara ya kampuni hiyo.
Amesema  kutoka na barabara kutokuwa muzuri kiwanda hicho kimekuwa kikisitisha uzalishaji wa saruji kutokana na kuwa na shehena kubwa kwenye maghala yao.
"Kwa muda sasa tuna shida ya barabara ya kuingia kiwandani huku jambo ambalo limekuwa likikwamisha usafirishaji hususani katika kipindi cha Mvua.
"Mzigo hautoki wala hatuingizi baadhi ya vitu muhimu katika kuendesha kuwanda kama vile makaa ya mawe hivyo kusababisha kodi ya serikali isipatikane ya kutosha, pia kuathiri wafanyakazi kwa kuchelewesha mishahara yao,"
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kimbiji Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour akipanda mti katika kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kimbiji Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour  akipata maelezo kwa Mhandisi wa Uzalishaji wa Kiwanda Lake Cement, Emmanuel Mayunga wakati Mwenge ulipofika katika kiwanda hicho .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Amour Hamad Amour akizungumza katika kiwanda lake Cement mara baada ya mwenge wa Uhuru kupita katika kiwanda hicho.
 Sehemu ya wafanyakazi wa Lake Cement wakifuatilia kinachoendelea wakati wa mwenge wa Uhuru ulipofika kiwandani hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa akizungumza katika Kiwanda cha Lake Cement wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita katika kiwanda hicho .

No comments: