Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Biashara Wilaya alilozindua rasmi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse).
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la Biashara.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba pochi iliyotengezwa kwa mkonge na kikundi cha wanawake wajasiliamali wilayani humo.
Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Kishapu wakifuatilia kikao hicho.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga, Dk. Meshack Kulwa akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (kushoto) akiangalia ngozi ghafi alipotembelea banda la kikundi cha wajasiliamali wa kutengeneza viatu cha Badimi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakiangalia viatu vilivyozalishwa na kikundi cha wajasiliamali Cha Badimi kilichopo wilayani humo.
Ofisa Biashara Wilaya ya Kishapu, Konisaga Mwafongo akichangia mada katika kikao hicho.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akizungumza wakati wa kikao.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Jumbe Samson akifafanua jambo wakati wa kikao.
Mashine ya kupura nafaka zikiwemo mtama iliyobuniwa na mwananchi wa Kishapu, Daudi Nkende ikiwa katika viwanja vya halmashauri kwa ajili ya maonesho ya wajasiliamali.
………………………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba amewataka Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kwenda sambamba na sera ya Tanzania yenye viwanda pamoja na kuimarisha uchumi wetu.
Amesema hayo wakati akizindua Baraza la Biashara Wilaya ambapo alishangazwa na baadhi ya kuamini kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini hazina ubora na hivyo kukimbilia za nje.
Talaba ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya alisema bidhaa zetu zina ubora kutokana na kutumia malighafi halisi akitolea mfano viatu vinavyozalishwa na Watanzania ukilinganisha na vinavyotoka nje ya nchi ambavyo vingi havidumu.
”Tufike mahali sasa tununue bidhaa zetu ili fedha izunguke kwani tutaimarisha uchumi na kama tunavyofahamu lengo la Rais katika sera ya nchi ya viwanda anataka tununue bidhaa zetu.
Mkuu huyo wa wilaya alilitaka baraza liwe chachu ya kusukuma sera ya nchi ya viwanda na kuibua fursa ambazo wananchi waananchi wanaweza kuzitumia na kuanzisha biashara.
Alilitaka baraza kuja na wazo mbadala la kibishara na kiviwanda ili wananchi waweze wawaunga mkono wajasirimali wadogo wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa wapate masoko.
Akifungua kikao cha kwanza cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Barazaa la Biashara Wilaya, Stephen Magoiga aliwataka wananchi kutumia vizuri fursa zilizopo wilayani humo.
Magoiga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu alisema tukitumia vizuri rasilimali zilizopo wilayani humo tutapiga hatua na kujenga historia.
”Tunapozungumzia viwanda siyo lazima viwe vikubwa hata vidogo vidogo mfano tunaweza kutumia kilimo kuibadilisha kabisa Kishapu na kuwa wilaya ya kwanza katika uchumi,” alisema.
Alitaja rasilimali kama madini na fursa za kilimo zilizopo wilayani humo kuwa kama zikitumika ipasavyo maisha ya wananchi yataboreka zaidi na uchumi kwa ujumla kuimarika.
Baraza hilo la biashara Wilaya ya Kishapu linaundwa na wajumbe 40 wakiwemo wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi na litadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment