Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017
Muonekano wa ukuta wa kanisa la KKKT Usharika wa Ubungolinalotakiwa kuvunjwa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo wakati wa kikao cha pamoja cha maridhiano ya utatuzi wa mgogoro wa Eneo la ardhi. Leo tarehe 23, Mei 2017
Darasa lililokabidhiwa na Uongozi wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ubungo kwa Uongozi wa Manispaa ya ubungo mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na Mchungaji kiongozi wa kanisa La Kiinjili la Kilutheli Tanzania Mchungaji Goodlisten Nkya alipozuru katika ofisi za kanisa hilo kwa ajili ya kikao na Uongozi wa (KKKT) Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017
Muonekano wa Majengo ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza yatakayofanyiwa marekebisho mara baada ya ujenzi wa Madarasa nane kukamilika
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza akizungumza na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo,Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa National Housing, Waalimu wa Shule ya msingi ubungo Plaza sambamba na viongozi wengine mara baada ya kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzuru kwa katika ofisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo leo tarehe 23, Mei 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017.
Na Mathias Canal, Dar essalaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo tarehe 23, Mei 2017 amefanya mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.
Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za usharika wa KKKT Ubungo kilikuwa na Agenda ya kujadili nanma bora ya uvunjaji wa Ukuta wa eneo la kanisa hilo ambao umeingia katika eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza Jambo linalopelekea Kushindwa kuanza ujenzi wa madarasa nane mapya kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao kwa sasa wanasoma katika madarasa ambayo majengo yake si rafiki kwa ajili ya usomaji.
Alisisitiza kuwa ujenzi huo utakuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alilolitoa Mei 19, 2017 wakati wa mkutano wake na walimu wa shule hiyo sambamba na wananchi wa Mtaa huo ukiwajumuisha Afisa mtendaji wa Kata na wajumbe wa mitaa.
MD Kayombo alisema kuwa baadhi ya shule katika Manispaa ya Ubungo hazifanyi vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa kutokana na uduni wa miundombinu ikiwemo madarasa Jambo ambalo pia limepelekea Manispaa ya Ubungo kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuwa rafiki kwa wanafunzi kujifunzia.
Alisema kuwa jukumu la viongozi wanaomuwakilisha Rais Magufuli katika ngazi za Mitaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na Taifa ni kusimamia na kutekeleza matakwa ya jamii kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi bila kumuonea mtu yeyote.
Aidha ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa ushirikiano waliouonyesha na kukubali kuwa na maridhiano ya pamoja kuhusiana na namna bora ya kutatua mgogoro huo ambapo pia amewaupongeza Uongozi wa KKKT Usharika wa Mabibo kwa kuamua kutoa moja ya jengo lao kwa ajili ya shule hiyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha miundombinu ya shule ili kukuza ufanisi wa elimu nchini.
Kwa upande wake mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo Mch Goodlisten Nkya amesifu uongozi wa Mkurugenzi Kayombo kwa kukubali kufanya maridhiano sambamba na kukubali kupokea jengo mojawapo la kanisa hilo walilotoa sadaka ambalo litatumiwa na shule ya Msingi Ubungo Plaza kama ofisi ya walimu ama darasa kwa kadri itakavyoamuliwa na uongozi wa shule.
Alisema kuwa adhma ya kanisa hilo ni kuona maendeleo endelevu ya elimu nchini Tanzania kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na kupongeza ushirikiano wanaoupata kutoka serikalini na katika Uongozi wa Shule hiyo.
No comments:
Post a Comment