Tuesday, May 23, 2017

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO

 Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.

 Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
 Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akizungumza katika mafunzo hayo.
 Ofisa Ugani kutoka Kata ya Luharanyogu, Aminiel John, akichangia mada.
 Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Buchosa, Nyabange Theopista akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa.
 Maofisa Ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
 Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.
 Mkutano ukiendelea.
 Usikivu katika semina hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Buchosa, Kelvin Rweitaka akifungua semina hiyo kwani niaba ya mkurugenzi.
 Taswira ya chumba cha mkutano.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.

Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

"Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.

Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.

Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.

Alisema hadi leo hii kuna mbegu bora moja tu inayotumika kwa wakulima ambayo aliitaja kuwa ni UKM 08 ambayo ikitunzwa na kuhifadhiwa vizuri itakuwa na  uwezo wa kutoa kilo 700 hadi 800 kwa ekari moja.

Alisema kuwa pamoja na kuwa na mbegu hiyo changamoto kubwa iliyopo bado haijawafikia wakulima wote wa zao hilo la biashara.

Chirimi aliwata wakulima wa zao hilo kuacha kufanya kilimo cha mazoea badala yake wafanya kilimo chenye tija kwa kufuata maelekezo ya watafiti na maofisa ugani.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange alisema matumizi ya bioteknojia katika kilimo ni muhimu katika uzalishaji wa mazao yenye tija.

Alisema nchi zinatotumia teknojia hiyo katika kilimo zimefanikiwa katika kilimo na kuwakomboa wakulima.

Alisema changamoto kubwa iliyopo kwa wakulima hapa nchini ni mazao yao kukumbwa na magonjwa kama mnyauko wa migomba, funza wa vitumba katika pamba, batobato na michirizi ya kikahawia katika mihogo na ukame ambao unasababisha mahindi kunyauka na kuwa tatizo hilo la ukame si kwa Tanzania pekee bali lipo na nchi za jirani za Afrika Mashariki.

Ofisa Ugani wa Kata ya Nyakalilo, Mariam Alex alisema katika kata yake changamoto kubwa ni wadudu waharibifu wa mazao ambapo licha ya kutumia dawa mbalimbali za kuwaua lakini bado hawajafanikiwa.

Alisema anaamini kupitia mafunzo waliopata kuhusu kilimo yanaweza kuonesha njia ya kukabiliana na changamoto hiyo kubwa waliyonayo.

No comments: