Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .
HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga imepata msaada wa wodi ya wazazi vyenye thamani ya sh. Milioni 65 kutoka kwaTaasisi ya Dhi Nureyn .
Akizungumza baada ya makabidhiano ya vifaa wodi ya wazazi , Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega amesema kuwa wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ilikuwa na hali mbaya kwa kukosa vitu muhimu ambavyo vinasababisha kupoteza maisha kwa mama au mtoto .
Amesema kuwa kutokana na wanawake wa Wilaya walikuwa hawana uhakika katika masuala ya uzazi lakini sasa suluhisho limepatikana kwa taasisi hiyo kutoa vitu hivyo katika kuokoa maisha ya mama na mtoto katika hospitali hiyo .
Ulega amesema kuwa kutokana tatizo hilo aliamua kwenda kuomba katika taasisi ya Dhi-Nureyn ambao waliangalia mahitaji katika wodi ya wazazi na kuamua kutoa msaada huo licha kuwa na changamoto zingine katika hospitali ya Mkuranga .
Nae Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi-Nureyn , Sheikh Said Abri amesema kuwa baada ya kupata maombi kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega juu ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga hasa katika kuokoa maisha mama na mtoto tuliona jambo la msingi kutekeleza.
Amesema kuwa wataendelea kuwa kusaidia kadri ya uwezo unapopatikana ili hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa kuwa na vifaa vinavyostahili katika kuhudumia wananchi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkuranga, Steven Mwandambo amesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka kutokana na vifaa hivyo kukosekana kwa muda mrefu huku mipango ilikuwa ikifanyika. Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhibiano ya vifaa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Mkuranga leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Dhi-Nureyn Mkoa wa Dar es Salaam, Mukhtari Iddi akisoma lisala juu ya juhudi zilizofanywa katika upatikanaji vifaa hiyo kutoka mfadhili wa Saudia Arabia, Salehe Al-Sheikh leo Mkuranga.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi-Nureyn,Shekh Said Abri akizungumza juu msaada huo waliotoa katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
Mshauri wa masuala ya Afya wa Taasisi ya Dhi-Nureyn, Dk Saleh Juma akitoa maelekezo jinsi vifaa walivyotoa vinavyofanya kazi yake katika kutoa huduma katika wodi ya wazazi .
No comments:
Post a Comment