Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja
na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (wa pili
kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB FANIKIWA
ACCOUNT leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi
Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB
FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James
Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus
Richard akiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua
jambo katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo
cha Biashara, Donatus Richard (kushoto)
BENKI
ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati
ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara
pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika
uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo
haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake
hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia.
Alisema
kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya
wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye
mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara,
James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika
kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha
katika kuendeleza biashara zao.
Alisema
Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na
taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara
wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'. Mkutano huo ukiendelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.
No comments:
Post a Comment