Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa tano
kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo
Dae es Salaam Jana April 22, 2017. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki
wa ujijirahaa blog
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa (wa nne
kulia) akigonganisha Glas zenye kinyaji cha shampeni na Wakuu wa
vitengo mbalimbali wa Hospitali hiyo
|
Baadhi
ya Wakuu wa Idara na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa
katika Gari kuelekea katika kusheherekea sherehe yao iliyofanyika Navy
Beach Kigamboni Dar es Salaam jana
Baadhi
ya wanakamati wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Segla Mgaya (wa tano kushoto) ambaye ni Afisa Muuguzi wa
hospitali hiyo
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH, Agnes Mtawa akizungumza
na wauguzi hao wakati wa kusheherehekea Get Together Party
2017 iliyofanyika Dar es Salaam jana April 22, katika Ukumbi wa Navy
Beach Kigamboni ambapo alipata nafasi ya kuanza kutowa salamu kutoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru
kwakutofika,
Mtawa alisema,
pokeeni salamkutoka kwa mpendwa wetu Mkurugenzi, anawasalimia sana na
kuwatakia heri katika sherehe hii na amesema Mungu akitupa uzima mwakani
anaomba taarifa apate mapema iliaweze kuserebuka nasi na kwakumalizia
salamu hizo alisema pia naomba mpoke salam zake
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kushoto) akipokea
Ua kutoka kwa mtunza hazina wa Kamati hiyo, Matilda Mrina ambaye ni
Afisa Mkuu Msaidizi Daraja la Kwanza
Meneja wa Jengo la Mwaisela, Unyanjite Hema akicheza mchezo wa karata na Muuguzi, Debora Bukuku wakati wa Sherehe hiyo
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa akizindua mchezo
wa mazoezi kwa kuruka kamba mbele ya Wauguzi (pichani hawapo) wakati
wa kusheherehekea, Get Together Party 2017 iliyofanyika Dar es Salaam
jana April 22, 2017 katika Ukumbi wa Navy Beach Kigamboni , ambapo
kulikuwa na michezo mbalimbali ya kuchangamsha mwili ikiwemo, kuruka
kamba, kucheza karata, kuogele, kucheza mpira na Burudani ya nyimbo
mbalimbali kutoka kwa kikundi cha wasanii cha wauguzi kutoka Hospitali
ya Taifa Muhimbili, michezo hiyo iliyoratibiwa na Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Segla Mgaya
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa pili kushoto) akisindikizwa na wauguzi hao na wapilikulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Segla Mgaya
Muuguzi wa Hospitali hiyo, Vaileth Minja akifungua Sherehe hiyo kwa Salaa
Wauguzi wakicheza |
Mkurugenzi Agnes Mtwa akicheza pamoja na wauguzi hao
Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa (mwenye mkanda mweusi tumboni) akionyesha umahiri wake kwa kucheza kwaito na wauguzi hao
Mwenyekiti wa Kamati hiho, Segla Mgaya akiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi hao
Meneja
wa Tawi la Benk NMB Muhimbili, (jina halikupatikana mara moja)
akizungumza na wauguzi hao akisisitiza, anaomba kushirikiana na Wauguzi
hao, hayo aliyasema wakati wa Sherehe ya Get Together Party
2017, iliyofanyika Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa Navy Beach
Kigamboni, alianza kwa kusema,
Sisi
wana wa NMB tunaamini kwa wafanyakazi wanapokutana kwa pamoja
wanaongeza ufanisi wa kazi kwa sababu wanakutana pamoja na wanapokuwa
Muhimbili kila mmoja anakuwa Bize na kazi yake, lakini hapa mnaweza
kubadilisha mawili matatu nakuweza kubadilisha mawazo, alisema
Sisi
wana wa NMB tunaimani wafanyakazi wa Muhimbili wana watoto, kwahiyo
tumewaletea bidhaa adimu ya mototo Akaunt ambayo unaweza kuifungua pale
kwetu katika Tawi letu lililopo Muhimbili, alisema
Ninaimani
pale kwetu tunavibanda kama sita ambavyo kuna wahudumu na ukifika pale
utamwambia muhudum unahitaji huduma hiyo na atakuletea fom na utaijaza
na kingine siolazima kwa wewe kuja Benk kuja kuweka pesa.
Utajazishwa
fom ambayo ikifika tarehe ambayo uliambia benk utakumbushwa na ile pesa
itatoka kwenye Akaun yako na itakwenda kwenye Akaut Mtoto. alisema
Menena huyo.
Huduma
hiyo nimbure kabisa kwani kwakufanya hivyo nikuwaandalia watoto wetu
msingi bora wa maisha na kuwaandalia ufanisi wao katika masomo yao ya
kila siku.
Karibuni sana na ninaomba tuendelee kushirikiana asanteni sana
Mkurugenzi
wa Uuguzi, Agnes Mtawa akiwaonyesha zawadi aliyokabidhiwa na Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Segla Mgaya (wa kwanza kulia) iliyo andaliwa wauguzi
hao
Afisa Muuguzi, Agnes Kaberege akifungua Shampeni
Mkurugenzi wa Uuguzi akiwasalimia wauguzi na kuanza kwa kumshukuru Mungu kwa kuwepo mahala hapa kwa siku ya leo,
Mtawa
alisema, nijambo la kihistaria mimi tangu niingie kufanya kazi hii
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili sikumbuki kufanya kitu kama hiki,
Kwakweli
nawashukuru kwa kubuni wazo kama hili na kwa sisi tuliyofika hapa na
ninajuwa wauguzi tupo wengi lakini niwachache walioitikia wito na
ninafikiri huu ni mwanzo mzuri,
Mungu
akitupa Uzima wakati mwingine hapa patakuwa hapana nafasi ya kucheza
pamoja na mvua nyingi lakini mmeweza kujitowa kwa kuja mahali hapa,
alisema Mtawa
Nawaomba
nduguzangu Wauguzi tuendelee kuwa na umoja kwa kushikamana kama
tulivyoonyesha siku ya leo, tuendelee kupendana, kupeana nguvu kwa
sababu kazi yetu kama mnavyo ijuwa kunachangamoto nyingi,
Lakini
tukiwa kama mahala kama hapa tunacheza na kufurahi ausio jamani? kwa
kuangalia Bahari na yale mabo mengine mengine tumeyaacha getini, kwahiyo
pamoja na shukrani nyingi nawaomba tufurahi kwa pamona, alisema Mtawa
kwa kumalizia ,
Leo si siku ya hutuba ni siku ya kufurahi
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi, Segla Mgaya (kulia) akimkabidhi zawadi
Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtawa,
wanaoshuhudia ni wanakamati
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia)
walio kaa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Sherehe hiyo
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia)
walio kaa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Sherehe hiyo
Mkurugenzi
wa Uuguzi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa tatu kulia)
walio kaa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benk ya NMB
No comments:
Post a Comment