Sunday, April 2, 2017

Wananchi shirikianeni na serikali ya awamu ya tano kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo 2025 – Balozi Seif Ali Iddi



Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga (kulia) akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda alipowasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017.
Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (mwenye miwani) akiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa Sherehe ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na wananchi (hawapo pichani) waliofika katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu toka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo ya mwenge wa uhuru 2017 kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi

Watoto wa alaiki wakitengeneza umbo la mlima Kilimanjaro na kuweka alama ya mwenge wa uhuru kuashiria kupandisha kwa mwenge huo katika mlima Kilimanjaro wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukabidhiwa mwenge huo kuukimbiza kwa siku 195 katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi akimpa mkono wa baraka kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour kabla ya kumkabidhi mwenge huo kuukimbiza katika mikoa 31 ya Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.

: Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto) akiwasha Mwenge wa Uhuru wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour (kushoto) akimhaidi mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi (kulia) kuulinda na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri zote 195 Tanzania bara na Zanzibari wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 Bw. Amour Hamad Amour akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa mwenge huo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kuukimbiza mwenge huo katika halmashauri 195 Tanzania bara na Zanzibar wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.
Watumbuizaji kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakitoa burudani wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru leo Mkoani Katavi.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi.





Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi 

Wananchi Mkoa wa Katavi wameombwa kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kujenga uchumi wa viwanda nchini. 

Rai hiyo imetolewa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Katavi na kusema kuwa Uchumi wa viwanda uliodhamiriwa ni ule utakaolifanya taifa kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani wa soko la kimataifa badala ya kuwa chanzo cha malighafi na soko la bidhaa za viwanda vya mataifa mengine. 

“Tanzania tumeazimia kutoka katika kundi la uchumi duni na kwenda kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda, Ujenzi na uimarisha wa viwanda nchini ambao utahusisha wadau mbalimbali wa Maendeleo, wananchi wenyewe, sekta binafsi na Mashirika Mbalimbali ya Kimataifa yanayo nafasi kubwa hususan katika uwekezaji mkubwa, ukuzaji wa mitaji, masoko, Teknologia na upatikanaji wa rasimali watu wenye ujuzi maalum” amesema Mhe. Balozi Iddi. 

Aidha Mhe. Balozi Iddi amesema kuwa wananchi wanayo fursa kubwa sana katika kujenga na kuendeleza viwanda nchini kwani ukuaji wa uchumi wa Viwanda unaanza kwa jitihada za wananchi wenyewe katika kuanzisha na kuendesha viwanda vidogo vidogo vinavyoweza kuongeza thamani ya mazao na bidhaa wanazozalisha kila siku katika maeneo yanayowazunguka. 


Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Katavi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mbio za mwenge wa uhuru zimekua zikihamasisha amani, mshikamano, kujenga uzalendo na umoja wa kitaifa kwa kuhamasisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ipo sambamba na malengo ya serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda kwa kufufua viwanda vilivyopo kuanzisha viwanda vidogo vidogo, viwanda vya kati na viwanda vikubwa. 

Mwaka huu, ujumbe mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unahusu Mkakati wa kukuza Viwanda nchini, chini ya Kauli Mbiu isemayo:- “Shiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu”. Ujumbe huu utaambatana na msisitizo wa Serikali kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa. 


Mwenge wa Uhuru uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika. Hatua hiyo ilikuwa ni utekelezaji wa ndoto yake iliyotafsiriwa kwa maneno aliyoyatamka mwaka 1958 kwa wajumbe wa Baraza la kikoloni la kutunga Sheria na kuyarudia tena mwaka 1959 alipohutubia kikao cha 35 cha Baraza la Umoja wa Mataifa wakati huo akidai Serikali ya madaraka kama Mbunge mwakilishi pekee wa Tanganyika kwa kusema “Sisi watu wa Tanganyika, tungependa kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike ndani na nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na heshima palipo jaa dharau”.Falsafa hiyo ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ujumbe mkubwa kwa Waingereza kwamba, watu wa Tanganyika wamechoka kutawaliwa. 

No comments: