JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
_________
TAARIFA
____
KUHUSU
UTEUZI WA WAGOMBEA
WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
______
1. Tarehe
17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku
ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30
Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku
ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa
Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.
2. Aidha,
natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa
nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la
mchakato wa uteuzi wa wagombea.
3. Vile
vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki
uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia
kubwa.
4. Pia
navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha
umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.
5. Kipekee
nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupitia vyama vyao
kugombea katika uchaguzi huu ambapo jumla ya Watu 505 walijitokeza kugombea kupitia vyama vifuatavyo:
A. CCM-
Wagombea-471;
B. CHADEMA-
Wagombea-17;
C. CUF-Wagombea-8;
D. NCCR-MAGEUZI-
Wagombea 3; na
E. ACT-WAZALENDO-Wagombea-6.
6. Wagombea
hao walichujwa na Vyama vyao na kupata majina ya watu 20 waliopitishwa kugombea
kwa mchanganuo ufuatao:
A. CCM-Wagombea
12;
B. CHADEMA-Wagombea
2;
C. CUF-Wagombea-4;
D. NCCR-MAGEUZI-Mgombea
1; na
E. ACT-WAZALENDO-Mgombea
1.
7. Kati
ya Wagombea hao Wanaume ni 12 na Wanawake ni 8 kwa Mchanganuo ufuatao:
A. CCM-Wanawake
6 na Wanaume 6;
B. CHADEMA-
Wanawake 0 na Wanaume 2;
C. CUF-Mwanamke
1 na Wanaume 3;
D. NCCR-MAGEUZI-Mwanamke
1 na Wanaume 0; na
E. ACT-WAZALENDO-Wanawake
0 na Mwanaume 1.
8. Majina
hayo ya Wagombea yaliwasilishwa na Vyama vyao kwangu tarehe 30 Machi, 2017
kabla ya Saa 10 Jioni kama masharti ya Kanuni ya 5(4) ya Nyongeza ya Tatu ya
Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.
9. Baada
ya hatua hiyo, nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha
na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 ya
Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Sheria
ya Uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5(1), (2) na (3)
ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Ufuatao
ni Mchanganuo wa maombi ya kugombea katika Makundi ya Uchaguzi:
KUNDI A: WANAWAKE
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Happiness Elias LUGIKO
|
KE
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
|
KE
|
CCM
|
KUNDI B: ZANZIBAR
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Abdullah Hasnu MAKAME
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Maryam Ussi YAHYA
|
KE
|
CCM
|
3.
|
Ndg.
Mohamed Yusuf NUH
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Ndg.
Rabia Hamid MOHAMEDI
|
KE
|
CCM
|
KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Ezekia Dibogo WENJE
|
ME
|
CHADEMA
|
2.
|
Ndg.
Habibu Mohamed MNYAA
|
ME
|
CUF
|
3.
|
Ndg.
Lawrence Kego MASHA
|
ME
|
CHADEMA
|
4.
|
Ndg.
Nderakindo Perpetua KESSY
|
KE
|
NCCR
|
5.
|
Prof.
Kitila MKUMBO
|
ME
|
A
CT
|
6.
|
Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO
|
KE
|
CUF
|
7.
|
Ndg.
Thomas D.C MALIMA
|
ME
|
CUF
|
8.
|
Ndg. Twaha Issa TASLIMA
|
ME
|
CUF
|
KUNDI D: TANZANIA BARA
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Adam Omari KIMBISA
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Anamringi Issay MACHA
|
ME
|
CCM
|
3.
|
Ndg.
Charles Makongoro NYERERE
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Dkt.
Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
|
ME
|
CCM
|
5.
|
Ndg.
Fancy Haji NKUHI
|
KE
|
CCM
|
6.
|
Ndg.
Happiness Ngoti MGALULA
|
KE
|
CCM
|
10.
Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka za uteuzi wa Wagombea
zilizowasilishwa na Chama cha Mapinduzi yanaonesha kuwa wagombea wote wamekidhi
vigezo na masharti ya uchaguzi. Ifuatayo ni orodha ya Wagombea hao katika
makundi waliyoomba kugombea:
I.
WAGOMBEA WALIOKIDHI
MASHARTI NA KUTEULIWA
KUNDI A: WANAWAKE
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Happiness Elias LUGIKO
|
KE
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
|
KE
|
CCM
|
KUNDI B: ZANZIBAR
NA.
|
JINA
|
JNSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Abdullah Hasnu MAKAME
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Maryam Ussi YAHYA
|
KE
|
CCM
|
3.
|
Ndg.
Mohamed Yusuf NUH
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Ndg.
Rabia Hamid MOHAMEDI
|
KE
|
CCM
|
KUNDI D: TANZANIA BARA
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg.
Adam Omari KIMBISA
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg.
Anamringi Issay MACHA
|
ME
|
CCM
|
3.
|
Ndg.
Charles Makongoro NYERERE
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Dkt.
Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
|
ME
|
CCM
|
5.
|
Ndg.
Fancy Haji NKUHI
|
KE
|
CCM
|
6.
|
Ndg.
Happiness Ngoti MGALULA
|
KE
|
CCM
|
II.
UTEUZI WA WAGOMBEA KATIKA KUNDI C -VYAMA VYA
UPINZANI
11.
Uteuzi wa Wagombea katika Kundi C (Vyama vya
Upinzani) haujafanyika kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwenye
nyaraka za uteuzi wa wagombea ambayo yanakiuka masharti ya Ibara ya 50 ya
Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ibara ya 67 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa
Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki ya Mwaka 2011 iliyotungwa na Bunge la
Afrika Mashariki. Muhtasari wa mapungufu yaliyobainishwa kwa Vyama husika ni
kama ifuatavyo:
1. CHADEMA
·
Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha
utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe
wa Bunge la Afrika Mashariki (The East
African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja
(1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either
gender).
·
Fomu za maombi ya wagombea hazipo.
·
Orodha ya waombaji haipo.
·
Fomu ya matokeo ya kura haipo.
2. CUF
·
Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha
utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe
wa Bunge la Afrika Mashariki (The East
African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja
(1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either
gender).
·
Fomu za Uteuzi wa Wagombea zimewasilishwa na
mamlaka mbili tofauti.
·
Wagombea wawili hawana uthibitisho wa Uraia.
·
Fomu ya uthibitisho wa hiari ya kugombea
haipo kwa wagombea wote.
·
Orodha ya waombaji haipo kwa Mgombea mmoja.
·
Fomu ya matokeo ya kura kwa wagombea wote
haipo.
·
Fomu ya Mahudhurio kwa mgombea mmoja haipo.
12.
Mapungufu hayo yamenifanya nishindwe kufanya
uteuzi wa Wagombea katika kundi hilo, hivyo nimeviandikia barua vyama vyenye
haki ya kugombea katika Kundi hilo kuvitaka kurekebisha mapungufu
yaliyobainishwa na kuwasilisha majina na nyaraka zinazohitajika ofisini kwangu
Dodoma Siku ya tarehe 4 Aprili, 2017 kabla ya saa 7:00 Mchana.
13.
Uteuzi wa Wagombea katika KUNDI C (Vyama vya Upinzani) utafanyika
tarehe 4 Aprili, 2017 wakati wowote kuanzia saa saba kamili (7:00) mchana mara
baada ya kupokea na kuchambua nyaraka zitakazowasilishwa kwangu na Vyama
husika.
14.
Kutokana na matokeo ya uchambuzi huo na kwa
kuzingatia masharti ya Ibara ya 50 ya
Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Masharti ya Ibara ya 67
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4(4) cha Sheria
ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Kanuni ya 12 ya Kanuni za
Kudumu za Bunge na Kanuni ya 5(1)(2) na (3) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za
Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 na Mwongozo wa Spika kuhusu Mgawanyo wa
Kura zinazotakiwa kupigwa katika kila Kundi, kwa mamlaka niliyopewa kama
Msimamizi wa Uchaguzi NATANGAZA na
kutoa TAARIFA kwa Umma kwamba,
wafuatao ndio waliokidhi vigezo na masharti ya kuteuliwa kugombea Uchaguzi wa
Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki uliopangwa kufanyika tarehe 4 Aprili, 2017
kwa mchanganuo ufuatao:
KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg. Happiness Elias LUGIKO
|
KE
|
CCM
|
2.
|
Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA
|
KE
|
CCM
|
KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg. Maryam Ussi YAHYA
|
KE
|
CCM
|
3.
|
Ndg. Mohamed Yusuf NUH
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI
|
KE
|
CCM
|
KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA
NA.
|
JINA
|
JINSIA
|
CHAMA
|
1.
|
Ndg. Adam Omari KIMBISA
|
ME
|
CCM
|
2.
|
Ndg. Anamringi Issay MACHA
|
ME
|
CCM
|
3.
|
Ndg. Charles Makongoro NYERERE
|
ME
|
CCM
|
4.
|
Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE
|
ME
|
CCM
|
5.
|
Ndg. Fancy Haji NKUHI
|
KE
|
CCM
|
6.
|
Ndg. Happiness Ngoti MGALULA
|
KE
|
CCM
|
Dr. Thomas D. Kashililah
MSIMAMIZI
WA UCHAGUZI
3 Aprili, 2017
No comments:
Post a Comment