Friday, April 14, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Askari nane wa jeshi la Polisi wameuawa na mmoja kujeruhiwa katika shambulio la kushtukiza lililofanywa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi mkoani Pwani. https://youtu.be/MTkJoCagIvo

SIMU.TV: Waumini wa dini ya kikristo nchini leo wameungana na waumini wenzao duniani kote kuadhimisha siku ya Ijumaa Kuu ikiwa ni kukumbukia mateso ya Bwana Yesu Kristo. https://youtu.be/PTgEws0sDZg

SIMU.TV: Wafanyabishara sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam wamelalamikia mwitikio mdogo wa wananchi katika kufanya manunuzi ya bidhaa kuelekea sikukuu ya Pasaka. https://youtu.be/138MDnRXN2s

SIMU.TV: Benki ya dunia imetoa mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni kumi na moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya taifa ya takwimu NBS makao makuu Dodoma. https://youtu.be/oVIsJw1HxJ4

SIMU.TV: Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule ameivunja bodi ya shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania TFC baada ya kubainika kuwepo kwa ubadhirifu. https://youtu.be/dSeNuSJOeGU

SIMU.TV: Operesheni maalumu ya kuondoa mifugo katika mapori na hifadhi za taifa mkoani Kagera imemalizika na kufanikiwa kukamata mifugo zaidi ya elfu tano na watuhumiwa 185. https://youtu.be/1hEvphEwrNE

SIMU.TV: Waziri mkuu wa zamani wa Israel Ehud Barack amelitaja eneo la Olduvai Gorge  lililopo katika hifadhi Ngorongoro kuwa eneo muhimu la makutano ya baina ya kizazi cha binadamu wa kale na sasa. https://youtu.be/3kx4jH_TrWU

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua miradi miwili ambayo ni  ule wa mabweni ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam na ule wa ujenzi wa nyumba za wananchi wa hali ya nchini katika eneo la Magomeni. https://youtu.be/TorO5UsUdz0

SIMU.TV: Wizara ya kilimo mifugo na uvuvi imeandaa muswada wa kuwasilisha bungeni ambao unaomtaka kila aneyejihusisha na kilimo kutumia wataalamu wa kilimo ili kuinua sekta hiyo. https://youtu.be/Btx_3nhZ-Hw

SIMU.TV: Timu ya taifa ya vijana Serengeti boys imeendelea na mazoezi katika kituo cha michezo mjini Rabat nchini Morocco ilikoweka kambi kujiandaa na fainali za vijana barani Afrika zitakazofanyika nchini Gabon. https://youtu.be/EleLxOxFyf8

SIMU.TV: Ligi kuu ya Tanzania bara inatarajiwa kuendelea tena mwishoni mwa juma hili kwa michezo mitano ambapo vinara wa ligi hiyo klabu ya Simba wataalikwa na Toto Afrika ya jijini Mwanza. https://youtu.be/Wgbd7PMIxlg

SIMU.TV: Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa klabu ya Yanga wanatarajiwa  kuingia uwanjani kesho huko nchini Algeria kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Mc Algers. https://youtu.be/DKRNw1lkDLw

SIMU.TV: Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amewalaumu washambuaji wa klabu yake baada ya kukubali sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Anderlecht kwenye mchezo wa robo fainali za kombe la Europa. https://youtu.be/owYjXRnoNNE\

SIMU.TV: Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar Es salaam limetangaza kuanza kwa Operesheni maalumu ya kuwasaka majambazi walioua Polisi wilayani Mkuranga; https://youtu.be/ovGHQ_jwSAg
SIMU.TV: Fuatilia mahojiano maalumu na Waziri wa mambo ya ndani nchini Mwigulu Nchemba kuhusu kuendelea kwa vitendo vya mauaji wa polisi nchini; https://youtu.be/7hI2IWVlU1o

SIMU.TV: Waumini wa dini wa Kikristo nchini wametakiwa kuwa wazalendo kwa kulinda nchi pamoja na Rasilimali zilizopo; https://youtu.be/Src25RGnfS0

SIMU.TV: Tume ya Taifa ya uchaguzi imemtangaza ndugu Getrude Lwakatare kuwa mbunge wa viti maalumu CCM kujaza nafasi ya Sophia Simba; https://youtu.be/83LFfWuKTi0

SIMU.TV: Mkurugenzi wa ofisi ya Takwimu Dr Albina Chuwa amemtaka msimamizi wa jengo la ofisi hiyo mkoani Dodoma kujenga kwa kuzingatia viwango bora; https://youtu.be/whjtZld08Sk

SIMU.TV: Baada ya Simba kupewa pointi tatu za mezani dhidi ya rufaa yao kwa Kagera Sugar, Yanga nao wamewaomba TFF kuwapatia pointi zao kutoka African Lyon; https://youtu.be/UupisF5weKs

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga Jumamosi hii itashuka dimbani huko nchini Algeria kurudiana na wapinzani wao klabu ya MC Alger ; https://youtu.be/R6_FORin8l0

SIMU.TV: Timu ya ngumi za ridhaa ya JKT iko katika maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya Ubingwa wa Taifa yatakayofanyika wiki ijayo jijini Dar Es salaam;  https://youtu.be/NDhTQANCkGU

SIMU.TV: Msanii machachari kwa sasa nchini Harmorapa anatarajia kupiga show kali katika mkesha wa Pasaka kwenye Ukumbi wa burudani Dar Live Mbagala; https://youtu.be/efeJxXilXlQ

SIMU.TV: Mchekeshaji maarufu kutokea nchini Kenya Emmanuel Nyambane amefariki dunia katika ajali mbaya iliyohusisha gari; https://youtu.be/x9Ou7xGgnc8

No comments: