Tuesday, April 4, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania bila kujali itikaji zao leo wamempokea rais mstaafu  Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa nderemo na vifijo alipokwenda kumshuhudia Mama Salma Kikwete akiapishwa kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. https://youtu.be/dDi4lXzIoPo

SIMU.TV: Serikali imesema itaendelea kushirikiana na nchi rafiki katika nyanja mbalimbali za uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa ili kufikia lengo la kuifanya nchi kuwa ya viwanda. https://youtu.be/XB7THwhfFQ8

SIMU.TV: Jukwaa la katiba Tanzania limeitaka serikali kutangaza upya katika gazeti la serikali kuhusu uanzishwaji wa mchakato wa katiba mpya. https://youtu.be/1Q7ce97kyYQ

SIMU.TV: Wadau wa mazingira wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kuinua uchumi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. https://youtu.be/ejgcAy9iPu4

SIMU.TV: Mamlaka ya uthibiti wa nishati na maji EWURA imetangaza bei mpya elekezi kwa mafuta ya petrol diesel na mafuta ya taa kutokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia. https://youtu.be/_a8s5-yIIKE

SIMU.TV: Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Dar es Salaam imeagizwa kufanya uchunguzi wa kina kufuatia kubainika kwa walipwa fidia hewa katika wilaya za Temeke na Ilala. https://youtu.be/4drrARCL16U

SIMU.TV: Kampuni ya JH Holding ambayo ni maarufu kwa utengenezaji wa karatasi nyeusi za vioo imefungua ofisi nchini ambayo itasaidia katika ulinzi wa mali. https://youtu.be/9KHdjNmzQJk

SIMU.TV: Tuzo za rais za mzalishaji bora wa viwandani zinatarajiwa kufanyika April nane ambapo makamu wa rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. https://youtu.be/XUAeHqYQsC4

SIMU.TV: Waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo Dr Harison Mwakyembe amekutana na waziri wa habari utamaduni sanaa na utalii wa Zanzibar Rashid Juma na kujadili namna ya kutatua migogoro katika vyama vya michezo. https://youtu.be/bZDzuFPp10k

SIMU.TV: Wapinzani wa klabu ya Yanga katika kombe la shirikisho kutoka Algeria Mc Algers wanatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamisi usiku. https://youtu.be/NQetkcNSEXk

SIMU.TV: Wizara ya habari sanaa utamaduni na michezo imeonya kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaovamia viwanja vya michezo na kujenga makazi. https://youtu.be/ssjzvx7-h6c

No comments: