Wednesday, April 26, 2017

RC NCHIMBI ABAINISHA KUSHINDWA KUMPATIA CHANJO MTOTO NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akitoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akifurahi mara baada ya kutoa chanjo kwa mtoto wa umri wa siku nne ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao waliojitokeza katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida wakishiriki uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akisoma hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo Mkoani Singida mapema leo katika hospitali ya Sokoine manispaa ya Singida.

………………………………………………………………………

Wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto kupata huduma za chanjo wanakiuka haki za binadamu hasa haki ya kuishi na pia wanaenda kinyume na juhudi za serikali za kupambana na maradhi, umaskini na ujinga.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesea hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Mwakilishi wake Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo uliofanyika mapema leo katika hospitali ya Sokoine Manispaa ya Singida.

Dkt. Nchimbi amesema watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano wanapaswa kupata chanjo zote ili kuwakinga na magonjwa ya homa ya ini, surua, nimonia, kuhara, kifua kikuu, na pepopunda ambayo yanazuilika kwa chanjo na motto akiugua kupona ni nadra

“Mtoto akiumwa magonjwa hayo kwa kukosa chanjo kupona ni majaliwa na akipona anaweza kupata ulemavu wa kudumu, hivyo nawasisitiza msipuuze mzingatie kukamilisha chanjo zote” amesisita

Ameongeza kuwa serikali imekamilisha wajibu wake kwa kuhakikisha chanjo zote zinapatikana na hivyo umebaki wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha motto anapata chanjo pamoja na kuwaelimisha na kuwafichua wale wasiowapeleka watoto kupata chanjo.

Akisoma taarifa ya hali ya chanjo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Salum Manyatta amesema Mkoa wa Singida kwa sasa una chanjo zote zinazohitaji na zinatolewa katika vituo 197 kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.

Dkt. Manyatta amesema kwa mkoa wa Singida wananchi wana uelewa wa chanjo ambapo kila mwaka zaidi ya asilimia 95 hufikiwa na chanjo karibia zote huku changamoto ikiwa ni katika kukamilisha chanjo ambazo huhitaji dozi zaaidi ya moja.

Ameongeza kuwa baadhi ya wazazi hujifungulia nje ya vituo vya kutolea huduma za afya mfano majumbani na hivyo kupelekea watoto kukosa chanjo za awali.

Dkt. Manyatta amesema katika kukabiliana na changamoto za baadhi ya watoto kukosa chanjo, jitihada zilizowekwa ni pamoja na kupitia kadi ya mtoto kuona endapo amekamilisha chanjo kabla hajapewa huduma nyingine za afya.

Jitihada nyingine ni viongozi wa serikali ngazi za vijiji kuandaa orodha ya watoto ambao hawajakamilisha chanjo na kuwafatilia wazazi au walezi wakamilishe chanjo hizo, kuendelea kutoa elimu na uhamasishaji wa chanjo na kutoa huduma ya mkoba na kliniki tembezi ili kuwafikia watoto wanaoishi maeneo ya vijijini sana.

Kauli mbiu ya wiki ya chanjo mwaka huu ni “Chanjo Humkinga Kila Mtu, Pata Chanjo”.

No comments: