Tuesday, April 4, 2017

Msikimbilie mikopo isiyokuwa na Tija – Mrajisi vyama vya Ushirika


Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona. Aliyeketi ni Kaimu Naibu Mrajisi Udhibiti na Usimamizi, Collins Nyakunga.
Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (Katikati) Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, Wakitia saini mkataba utakao iwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona.


Kaimu Mrajisi wa Vyama vya ushirika nchini, Tito Haule amevitaka vyama vyote vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha, ambayo inavighalimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo halisi wa vyama husika na kuwaingiza wanachama wao katika matatizo kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo huku akiwashauri kuangalia huduma ambazo zinawalenga wananchi moja kwa moja.

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati wa kusaini makubaliano na Benki ya Wanawake ya Covenant ambayo yataiwezesha benki hiyo kuweza kutoa huduma mbalimbali za bima pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini, Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma Mrajisi ameitaka benki hiyo kuhakikisha inatimiza adhma ya kutoa huduma ambazo zitawanufaisha wanachama moja kwa moja na sio viongozi wachache.

“Vyama vingi vimekuwa na mazoea ya kujiingiza katika mikopo mikubwa na wakati mwingine hata kuzidi uwezo halisi wa vyama husika, lakini pia viongozi wanaokuwepo wanakuwa sio waaminifu na kujikuta wanashindwa kusimami matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu na kujikuta wanaviingiza vyama katika matatizo makubwa,” alisema Haule na kuongeza kuwa, “Ninawsaihi viongozi waache utaratibu huu ambao umeendelea kuvifanya vyama vya ushirika kushindwa kuwa sehemu ya ukombozi wa wanachama wake bali sehemu ya kuwakandamiza,”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo utakao iwezesha benki hiyo kufika maeneo mbalimbali nchini kutoa huduma kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini amesema atahakikisha benki yake inafanya kazi waliyokubaliana na msimamizi huyo wa vyama vya ushirika kwa uaminifu na weledi ili kuweza kuwainua wanachama wa vyama vya Ushirika.

“Tumefanya utafiti kwa muda mrefu sasa, kuangalia namna ambavyo tunaweza kuwasaidia wajasiriamaliwadogo miongoni mwao wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na wafanya biashara, tumegundua wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa huduma za Bima ya matibabu pamoja na ajali, hivyo tumeanzisha huduma hizo ili kuwaondolea mzigo ambao wanaupata kila siku wanapopata fedha wanashindwa kuweka akiba,”

Mkurugenzi huyo alihitimisha kwa kumshukuru mrajisi kuwapatia ruhusa ya kuhudumia vyama vya Ushirika nchini na kusisitiza kuwa watatoa ushirikiano kwa ofisi hiyo ili kuhakikisha mamilioni ya wanachama wa vyama vya ushirika wananufaika moja kwa moja na huduma zitakazo tolewa na benki hiyo.

No comments: