Wednesday, March 1, 2017

WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA TAMASHA LA KUMBUKIZI LA VITA VYA MAJIMAJI NA KUZINDUA MAKUMBUSHO YA HAYATI DR. RASHID MFAUME KAWAWA MJINI SONGEA

 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof.Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na wananchi kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge ( wa pili kulia) Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma, Jacquiline ngonyani ( wa kwanza kulia) Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke ( wa kwanza kushoto) pamoja na Chifu wa wangoni, Emanuel Zulu (wa pili kushoto) . Picha na Lusungu Helela- WMU)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa akitunukiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa katika kulitumikia taifa kwa uzalendo mara baada ya kuzinduzia jana Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Picha na Lusungu Helela- WMU)
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akizungumza na mtoto wa wa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Vita Kawawa ( wa kwanza kushoto) mara baada ya kuangalia baadhi ya vitabu vya Hayati Kawawa alivyokuwa akivipenda kuvisoma enzi za uhai wake vilivyopo katika Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa baada ya kuzindua makumbusho hayo iliyofanyika jana mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe akiweka silaha ya jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya SongeaBalozi wa Ujerumani nchini Tanzania
 Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma (CCM) Jacquline Ngonyani akiweka silaha ya jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya SongeaBalozi wa Ujerumani nchini Tanzania
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe ( wa tatu kulia) akiwa na Chifu wa Kabila la wangoni, Emmanuel Zulu ( wa pili kulia) wakiwa kwenye maandamano ya siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mwenyekiti wa Machifu wa nchini, Chifu Fundikila (kulia) pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke ( wa pili kushoto) . Picha na Lusungu Helela- WMU)

No comments: